MLINDA MLANGO WA AC BONGOVILLE ‘SYLVAIN AZOUGOUI’ AFARIKI DUNIA

Mlinda mlango wa klabu ya AC
Bongoville ‘Sylvain Azougoui’
amefariki dunia mara baada ya
kuumia kichwani wakati wa mchezo
wa ligi kuu huko Gabon.

image

Sylvian Azougoui

Kipa huyo Raia wa Togo mwenye
umri wa miaka 30 alifikwa na umauti
akiwa njiani kukimbizwa hospitalini
baada ya kutokea kwa tukio hilo,
wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya
Centre Mberi Sportif.

image

Taarifa zimesema Azougoui
alikumbana na mkasa huo wakati
akizuia moja ya shambulizi langoni
mwake lakini kwa bahati mbaya
aligongana katika eneo la kichwa na
mshambuliaji wa timu pinzani, hali
iliyopelekea kufikwa na umauti.
Familia ya mpira wa miguu ya
Gabon, imetoa pole kwa familia ya
marehemu ambayo ipo Togo pamoja
na klabu yake kwa ujumla bila
kusahahu shirikisho la soka la Togo
ambapo goli kipa huyo anatokea.

By Poldavy Selassie Posted in SPORTS

Hii ndio ndinga mpya aliyonunua Davido kwa zaidi ya Tsh milioni 200

Amepata nomination 4 kwenye MTV
Africa music awards 2014 na pia ana
mashabiki wengi barani Africa na nje
pia kitu ambacho kinamfanya asitulie
kila siku anazunguka nchi tofauti
akifanya show.
Hayo yote na faida nyingine za
muziki zinampa kila sababu Davido
kununua vitu avipendavyo kama
magari kutokana na mapato hayo.
Mwaka jana alinunua Mercedes Benz
G-Wagon yenye thamani zaidi ya Tsh
milioni 300 na hivi sasa amenunua
gari ya kisasa ya mwaka 2014
Mercedes Benz S63AMG yenye
thamani zaidi ya Tsh milioni 200.

image

Wasanii wa Afrika Mashariki wapanga kuzisusia tuzo za MAMA!!

Website ya Nairobi News imeripoti
kuwa wasanii wa Afrika Mashariki
wanapanga kuzisusia tuzo za MTV
Africa Music Awards, MAMA.

image

Diamond ni msanii pekee wa
Tanzania aliyetajwa kuwania tuzo
hizo mwaka huu
Wasanii hao wanazishutumu tuzo
hizo kwa kutozitendea haki nchini za
Afrika Mashariki mwaka huu na kwa
kuwapendelea wasanii wa Afrika
Kusini na Nigeria zaidi. “Uganda
imeumia zaidi kwasababu kutajwa
kwao pekee ni kwa collabo na
Amani,” msanii mkubwa wa Kenya
ambaye hakutaka kutajwa jina lake
aliuambia mtandao huo.
Umeandika kuwa wasanii
waliotarajiwa kutajwa kwenye tuzo
hizo ni AY, Ommy Dimpoz na Lady
Jaydee, Tanzania, P-Unit, STL, Elani
na Wyre wa Kenya na Jose
Chameleone na Navio wa Uganda.
Mtandao huo umeripoti kuwa wasanii
wengi zaidi wanapanga kutoshiriki
kwenye show za utangulizi za Road
to Mamas zitakazofanyika Dar es
Salaam kwa Afrika Mashariki

Sudan Kusini:Mauaji ya kikabila Bentiu

image

Waasi nchini Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa unasema kuwa
vikosi vinavyoipinga serikali nchini
Sudan Kusini viliwaua mamia ya
watu kwa sababu ya kabila lao
wakati vilipouteka mji wa Bentiu wiki
jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo,
watu hao walilengwa wakiwa katika
maeneo salama walikokuwa
wanahifadhiwa kama vile msikitini,
makanisani na hospitalini.
Umoja huo umesema kuwa
watangazji katika baadhi ya vituo vya
redio walitumia lugha ya chuki na
uchochezi na kuwataka watu wa
kabila fulani kuondoka mjini humo
huku wakiwashauri wanaume
kuwabaka wanawake.
Watu wa kabila laNuer, ni wafuasi
wakubwa wa kiongozi wa waasi na
makamu wa zamani wa Rais Riek
Machar
Wapiganaji wanaomuunga mkono
makamu wa rais wa zamani Riek
Machar waliuteka mji wa Bentiu
ambao ni mji mkuu wa jimbo la Unity
siku sita zilizopita.
Walinda amani wa Umoja wa
Mataifa walilaani kile walichokitaja
kama mauaji yanayowalenga raia
kwa misingi ya ukabila.
Rais Salva Kiir anatoka kabila la
Dinka ambalo ndilo kabila kubwa
kuliko yote nchini Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa umesema kuwa
watu ambao hawakuwa wa kabila la
Nuer,waliuawa Bentiu.
credit: BBC

Mbunge auawa na Al Shabaab Mogadishu

image

Gari ambalo lilikuwa na bomu
lililokuwa limetegwa na Al Shabaab
Mbunge mmoja ameuawa katika
shambulizi la bomu lililokuwa
limetegwa ndani ya gari mjini
Mogadishu Somalia.
Kundi la wanagmabo la Al Shabaab
limekiri kufanya shambulizi hilo dhidi
ya mbunge Isak Mohamed Rino.
Mbunge mwingine Mohamed Ali,
alijeruhiwa katika shambulizi hilo
ambalo limetokea huku serikali ikiwa
mwenyeji wa kongamano la
usalama.
Wanajeshi wa serikali wameweza
kupiga hatua dhidi ya wapiganaji wa
al-Shabaab katika siku za hivi
karibuni , lakini kundi hilo bado
linadhibiti maeneo mengi ya Kusini
mwa Somalia.
Waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed,
amelaani shambulizi hilo na kulitaja
kama kitendo cha uoga.
Rais Hassan Sheikh Mohamud
mnamo siku ya Jumapili, alifungua
rasmi kongamano hilo akisema kuwa
tabia ya mashambulizi ya kiholela
ambayo yamegubika Somalia kwa
miaka 23 lazima ikome.
Kundi la Al-Shabaab hufanya
mashambulizi ya mara kwa mara ya
kuvizia mjini Mogadishu na katika
maeneo mengine ya nchi hiyo.
Somalia imekuwa ikikumbwa na vita
vya wenyewe kwa wenyewe tangu
mwaka 1991 wakati Siad Barre
alipopinduliwa.

Rais wa Korea Kusini alaumu nahodha

image

Juhudi za uokozi zingali zinaendelea
Rais wa Korea kusini Park Geun Hye
amemkosoa nahodha na wafanyikazi
wa Feri ya abiria iliozama kwa
kuikimbia feri hiyo na hivyobasi
kufananisha vitendo vyao na mauaji.
Matamshi ya rais Park yanafuatia
uchapishaji wa mawasiliano kati ya
feri hiyo na waokozi ,yaliobaini
kwamba kulikuwa na hali ya
wasiwasi mbali na kutokuwepo
mpangilio wa uokozi.
Idadi ya watu waliofariki
imeongezeka na kufikia 64 huku watu
238 wakiwa hawajulikani
waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi
wa shule.
Wapiga mbizi wanaendelea na juhudi
za kutafuta mili ya watu waliozama
na feri hiyo huku wakijitahidi kuingia
ndani ya feri yenyewe.
Habari zilizotangazwa kuhusu
mawasiliano ya mwisho kati ya
wafanyakazi wa Feri iliyozama Korea
Kusini na maafisa wa kudumisha
usalama baharini zinaonyesha kuwa
kulitokea hali ya wasiwasi kabla ya
mkasa huo, ambayo huenda
ilichangia pakubwa vifo vya abiria
wengi katika feri hiyo.
Taarifa hiyo mpya ilitolewa Jumapili
alasiri wakati ambapo
imethibitishwa kuwa maiti 62
zimepatikana kwenye mabaki ya feri
hiyo, na kufanya idadi ya watu
waliothibitishwa kufariki kufikia 58.
Zaidi ya watu 240 hawajulikani
waliko hivi sasa.

image

Jamaa wa waathiriwa walikabiliana
na polisi wakilaumu waokozi kwa
kujikokota
Jamii za watu ambao hawakuwa
wamepatikana walifanya maombi ya
Pasaka Jumapili katika chumba cha
kufanyia mazoezi katika eneo la
Jindo, ambako mamia ya watu
wamekusanyika tangu feri hiyo
kupinduka wakisubiri habari
kuwahusu wapendwa wao.
Mama mmoja alisema kuwa watoto
waliofariki walikuwa wakitunzwa
vizuri.
“Naamini watoto hao wako
mbinguni ,” mama huyo alisema.
Jung Maria, mwanamke aliyejitolea
kuzisaidia familia za walioathirika,
alisema kuwa jamaa za watu
wasiojulikana waliko wanapaswa
kusikia kilichotokea kwa njia moja au
nyingine.
“ikiwa wamefariki, tunapaswa kupata
miili yao haraka iwezekanavyo. Na
iwapo kutatokea muujiza basi
turejeshewe watoto hao upesi pia,
alisema mfanyakazi huyo wa
kujitolea
Idadi kubwa ya abiria katika meli hiyo
walikuwa wanafunzi wa shule ya
upili waliokuwa wakienda kwenye
mojawapo wa kisiwa kubarizi. Hadi
kufikia sasa kumekuwa kungali kuna
ubishi mkubwa iwapo nahodha
mwenyewe alikuwa ameshikilia
sukani.

By Poldavy Selassie Posted in NEWS

Hii Ndio Video Ya Izzo Bizness Inayochezwa Channel O Kwa Sasa

Ni furaha na hatua kubwa kwa
msanii wa Tanzania kuona na
kusikia kazi yake ikipewa nafasi
kwenye vyombo vya habari kama
radio na tv vya nje ya Africa
mashariki kwani ubira wa hali ya juu
wa kazi hizo ndio huchangia zaidi
kazi hio kukubalika. Video ya wimbo
wa Izzo Bizness – Tumoghele ft
Hance Puff imeanza kuchezwa
channel O.
Kwenye video hii anaonekana video
model wa Tanzania Sabrina na
rapper/singer Quick Rocka.

image

image

Izzo aliandika maneno haya
yaliyoambatanishwa hii hii picha
“Hakika MUNGU ni mwema huu ni
mwanzo mzuri shukrani zangu za
dhati kwa wazazi wangu, @
masterjtz@shaa_tz@skywalkertz@
chokadj@bdozen@aytanzania#
joket@the_real_njobe@quickrocka
Na wote mliosupport na
mnaoendelea kusupport Pia shukrani
zangu za dhati kwa Director wa video
@nickdizzorusule@nickdizzorusule@
nickdizzorusule@nickdizzorusule
naomba tuzidi kuirequest izidi
kufanya vizuri…Sasa tumefika @
channeloafrica@channeloafrica@
channeloafrica@channeloafrica“

Kama ilikupita basi hii ndio video
yenyewe

Makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya 1,000 yakamatwa China

Wakati ziara ya dunia ya kikombe
halisi cha kombe la dunia ikiendelea
kabla ya kukabidhiwa kwa mmiliki
wake mpya ambaye ni mshindi wa
mwaka huu huko Brazil, maafisa wa
China wamekamata makombe feki ya
kombe la dunia zaidi ya 1,000,
yaliyokuwa yamedhamiriwa kuuzwa
katika kona mbalimbali za dunia.

image

makombe feki
Ikiwa zimebaki siku chache kabla
kombe la dunia 2014 halijaanza
kutimua nyasi huko Brazil , maafisa
wa forodha wa China wamekamata
makombe hayo ya dhahabu 1,020
huko katika mji wa Yiwu yakiwa
tayari kusafirishwa kuelekea Libya
kuuzwa, na kabla ya hapo makombe
mengine feki 1,008 yalikamatwa.

image

Kwa kuyatazama makombe hayo feki
yanafanana sana na kombe halisi la
dunia.

image

kombe halisi la dunia
Kombe halisi la dunia pia lilikuja
Tanzania mwishoni mwa mwaka
jana 2013.
Source: Mail Online

RAIS BARACK OBAMA AMKARIBISHA MAKAMU WAKE KWENYE ULIMWENGU WA SELFIE NA INSTAGRAM

Katika kuonyesha kunogewa na
mtindo mpya wa picha ‘SELFIE’. Rais
wa marekani Barack Obama
amemkaribisha makamu wake wa
Rais ‘Joe Biden kwenye mtandao wa
Instagram kwa staili ya kupiga picha
‘Selfie’ pamoja iliyowekwa kwenye
akaunti rasmi ya kiongozi huyo
ambayo ina wafuasi wapatao Laki 1
na ushee.

image

Rais Barack Obama na Makamu
wake wa Rais Joe Biden
wakitokelezea katika SELFIE.
”Found a friend to join my first selfie
on Instagram. Thanks for following
and stay tuned. –VP” aliandika Biden
kwenye ukurasa wake wa Instagram,
wakati Obama aliandika ”Welcome
to Instagram, Mr. Vice President.”
kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Unaweza ukatazama picha nyingine
zaidi za makamu huyo wa Rais
alizokwisha kuziweka kwenye
ukurasa wake tangu ajiunge rasmi na
Insta Aprili 16 mwaka huu, akiwa
tayari ameshapakia picha tano ndani
ya kipindi cha siku 3 tu. Chezea insta
wewe