MIRAJI KIKWETE AAGA UKAPERA


kikwete+clip[1]
Shamra shamra na nderemo zilitawala jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City wakati Miraji Kikwete, mtoto wa Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete alipofunga ndoa na Alma Mahmoud.

Sherehe hizo zilianza saa 7:00 mchana baada ya ndoa kufungwa na maharusi hao kuingia ukumbini hapo wakiongozana na Rais Kikwete.

Hali nje ya ukumbi huo ilikuwa tulivu ingawa uwanja ulikuwa umefurika magari ya polisi, viongozi na wageni waalikwa. Huku kikosi cha kudhibiti ulinzi na usalama kikiwa kimefunga mitambo ndani na nje ya ukumbi huo.

Ulinzi katika eneo hilo ulikuwa ni mkali kupita kiasi ambapo hakuna yeyote aliyeruhusiwa kuingia ukumbini humo bila kadi maalumu, hata angeomba kwa kupiga magoti.

“Hata sisi tumetoka Bagamoyo hadi hapa tuna undugu kabisa na mkubwa (Rais Kikwete), lakini wametunyima kwa sababu hatuna kadi,” alilalamika mwanamke mmoja aliyeongozana
na wanaume wawili.

Hakuna waandishi wa habari walioruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi huo, isipokuwa waandishi na wapiga picha maalumu wa Serikali…

View original post 346 more words