TANGAZO MAALUM KUTOKA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO


    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO                                                                     TANGAZO Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, inawaalika Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kote nchini kushiriki katika kikao kazi kitakachofanyika katika Hotel ya Tanga Beach Resort kuanzia Februari 3 hadi 8, 2014 Mkoani Tanga. Washiriki wote wanakumbushwa kulipa ada ya ushiriki kabla ya tarehe 30 Januari, 2014. Kauli… Continue reading TANGAZO MAALUM KUTOKA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

Muswada wa Sheria ya Wagudunzi wa aina mpya za mbegu wajadiliwa Visiwani


Mwakilishi wa jimbo la Kitope Makame Mshimba Mbarouk akichangia Mswada wa Sheria ya kuanzisha sheria za Hakimiliki za wagunduzi wa aina Mpya za Mbegu za Mimea katika Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar. Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu akichangia Mswada wa Sheria ya kuanzisha sheria za Hakimiliki za wagunduzi wa aina Mpya za Mbegu za Mimea katika Baraza… Continue reading Muswada wa Sheria ya Wagudunzi wa aina mpya za mbegu wajadiliwa Visiwani

Daraja la Dumila lasombwa na maji baadhi ya majengo ya Shule yafunikwa.


Habari zilizopatikana mchana huu zinasema kuwa Daraja la Dumila lililopo mkoani Morogoro ambalo ni barabara ya Dodoma – Morogoro limekatika na magari hayapiti baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia leo. Baadhi ya magari yatokayo upande wa Dodoma na Morogoro yameamua kugeuza na kurudi yalipotokea maana hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo. Kutokana na mvua hiyo madarasa katika Shule ya Msingi Magole, Dumila, Morogoro… Continue reading Daraja la Dumila lasombwa na maji baadhi ya majengo ya Shule yafunikwa.

RAIS KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MATUMIZI YA RASILIMALI ZETU .


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini waliohudhuria Kongamano la siku mbili linalohusu Rasilimali za Gesi Asilia, Mafuta na Madini kwa Amani na Maendeleo ya Tanzania linalofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam tarehe 20 -22, Januari 2014. Continue reading RAIS KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MATUMIZI YA RASILIMALI ZETU .