Hip-Hop Rumors: Did Kindness Turn Into Beef For Nicki Minaj?


Advertisements

Tundu Lissu amng`ang`ania Zitto Kabwe.


0044Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema hakuna wanachama wala kiongozi yeyote atakayejiona ni mkubwa zaidi ya chama kiasi cha kumfanya asichukuliwe hatua anapokiuka maadili ya chama.

Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, Lissu alisema chama kitaendelea kushusha mjeledi kwa wanachama na viongozi wake watakaobainika kwenda kinyume na maadili na katiba ya chama.

Lissu ambaye alikuwa akielezea uamuzi uliochukuliwa dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, alisema Chadema ni chama cha siasa na siyo taasisi binafsi, hivyo ni lazima katiba yake iheshimiwe.

“Chadema ni chama cha siasa na siyo taasisi binafsi, na kwa kuwa sisi ni chama cha siasa, tuna katiba, tuna kanuni, miongozo na kuna vikao halali,” alisema Lissu.

Aliongeza kuwa lengo la chama ni kusimamia maadili ya chama ili isije ikajengeka tabia kwamba kuna baadhi ya watu ambao wako juu ya…

View original post 99 more words

MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA WAKULIMA MOROGORO


Breaking_News-300x178MABOMU ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa – Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji.

Wakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali sehemu za siri na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha msongamano mkubwa wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa.

Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.

Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu…

View original post 12 more words