Tundu Lissu amng`ang`ania Zitto Kabwe.


0044Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema hakuna wanachama wala kiongozi yeyote atakayejiona ni mkubwa zaidi ya chama kiasi cha kumfanya asichukuliwe hatua anapokiuka maadili ya chama.

Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, Lissu alisema chama kitaendelea kushusha mjeledi kwa wanachama na viongozi wake watakaobainika kwenda kinyume na maadili na katiba ya chama.

Lissu ambaye alikuwa akielezea uamuzi uliochukuliwa dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, alisema Chadema ni chama cha siasa na siyo taasisi binafsi, hivyo ni lazima katiba yake iheshimiwe.

“Chadema ni chama cha siasa na siyo taasisi binafsi, na kwa kuwa sisi ni chama cha siasa, tuna katiba, tuna kanuni, miongozo na kuna vikao halali,” alisema Lissu.

Aliongeza kuwa lengo la chama ni kusimamia maadili ya chama ili isije ikajengeka tabia kwamba kuna baadhi ya watu ambao wako juu ya…

View original post 99 more words