MWIGULU AWATOLEA UVIVU VIONGOZI WA UMMA.


Mwigulu Nchemba1[1]
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ametoboa madudu aliyoyaona kipindi kifupi alichokaa kwenye ofisi hiyo baada ya kuapisha hivi karibuni.

Alisema amegundua sheria ya ununuzi ni uchochoro wa wizi wa kistaarabu unaotishia ustawi wa taifa.

Mwigulu alisema ni wizi wa kutisha kuona mtu binafsi akinunua soksi dukani analipa Sh2,000, lakini akitumia sheria ya ununuzi soksi ya aina ile ile itanunuliwa kwa Sh80,000.

Alisema sheria hiyo ni mzigo mzito kwa Serikali na kutoa mfano mwingine kwamba, waziri mmoja alikwenda safari ya kikazi nje ya nchi, lakini aliamua kwenda na mkewe kwa gharama zake alimlipia Sh1 milioni, lakini yeye kwa utaratibu sheria ya ununuzi alilipiwa na Serikali tiketi ya Sh4 milioni wakati walikuwa ndege moja na viti vinavyofuatana.

Mwigulu alisema hayo juzi jioni alipozungumza na wafanyabiashara jijini hapa kupitia Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), huku wakimweleza kuwa sera mbaya ya kodi ndiyo inayosababisha watu wengi kukwepa ulipaji kodi.

‘Nakiri…

View original post 212 more words