TETESI : JANET JACKSON AFIKIRIA KUDAI TALAKA KWA MUMEWE BILIONEA WISSAM AL MANA.


larrybway91

Wissam Al Mana and Janet Jackson attend Kira Plastinina's fashion show on October 25, 2012 in Moscow, Russia. Tetesi zilizoenea kwenye vichwa vingi vya habari na mitandao ni kuhusu hatima ya ndoa kati ya mwanamuziki wa Marekani Janet jackson na mumewe ambaye ni bilionea Wissam Al mana kuonekana kuingia doa…

Chanzo kimoja maarufu cha habari za mastaa kilidai kwamba Janet anafikiria kudai talaka pamoja na malipo ya ndoa hiyo iliyofungwa kwa mkataba maalum(Prenup) huku sababu kuu ikitajwa kuwa ni mumewe kuwa bize na shughuli zake za kibiashara ambazo humlazimu kusafiri kila mara  na kumuacha Janet akiwa mama wa nyumbani  hivyo kukosa muda wa kutosha wa kuwa pamoja..

Awali Janet aliwahi kuolewa mara mbili,  ndoa ya kwanza na James SeBarge na ya pili na  Rene Elizonda pia aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu na producer na rapa  mkongwe Jermaine Dupri.

View original post