Vita ya uenyekiti Bunge la Katiba


chengesitta Kadiri siku zinavyosogelea uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, ndivyo mpasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unavyozidi, kutokana na kuwapo kwa makundi mawili yanayojipanga kusimamisha wagombea na ambayo yameanza kuendesha kampeni kuchafuana.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa makundi hayo ni yale yanayomsaidia aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambao wametajwa kutaka kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, wakati Chenge akiwa hayuko tayari kuthibitisha nia yake hiyo, Sitta hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo. Lakini habari zinasema vigogo hao wameshajipanga kwa ajili ya mbio hizo za uchaguzi na sasa wanatafuta watu wa kuwasaidia.

Makundi hayo yalianza wakati wa kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, ambako habari zilisema, baada ya chama kumteua Pandu Ameir Kificho kuwania nafasi ya mwenyekiti wa muda wa Bunge la Katiba, mmoja wa wajumbe wa kikao hicho walimpendekeza Chengeā€¦

View original post 545 more words

Advertisements