OKOCHA AJUTIA KUKOSA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA KATIKA HISTORIA YAKE YA MPIRA.


larrybway91

Aliyekuwa kiungo mkabaji wa kikosi cha Super Eagles ‘Nigeria’, Jay Jay Okocha, amesema kwamba anajutia kitendo cha kukosa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika inayotolewa kila mwaka na shirikisho la mpira Africa(CAF) katika historia yake ya mpira.

Akiongea na mashabiki wake,  staa huyo alisema kwamba ”Najutia kitendo cha kukosa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika,  nilitegemea ningeweza kupata kipindi nipo kwenye fomu lakini wakati mwingine sio kila kitu unachopanga huenda kama ulivyotarajia,  shukrani kwa CAF,  kwani niliweza kutambulika na kupata tuzo nyingine tofauti na hiyo.

View original post

Advertisements