Meek Mill Takes Over Hollywood At Supperclub


Advertisements

SAFARI YA KUELEKEA AFRICA MAGIC VIEWERS CHOICE AWARDS(AMVCA) 2014.


larrybway91

Ni takribani mwezi mmoja umebakia wa kushuhudia kutolewa kwa tuzo za Waigizaji bora barani Afrika zinazofahamika kwa jina la AMVCA –Africa Magic Viewers Choice Awards itakayodhaminiwa na kinywaji cha Amstel Malta na hivyo kuwapa fursa mashabiki kuweza kuwapigia kura mastaa wanaowaona wanastahili kupata tuzo hizo.

Kwa hapa nyumbani kwetu Tanzania,  tunawakilishwa na muigizaji wa Tamthiliya ya Siri ya Mtungi,  Juma Rajab Rashid a.k.a Cheche akiwania tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume kwenye Tamthilia/Dramaakishindana na waigizaji kama vile Majid Michel,  Hlomla Dandala na Tope Tedela..Watanzania wenzangu itapendeza sana kusikia tuzo hiyo inakuja Tanzania, kwa kumpigia kura mshiriki wetu  Juma Rajab Rashid ili aweze kuibuka mshindi…Kwa taarifa zaidi jinsi ya kuweza kumpigia mshiriki wako kura,  Tembelea tovuti hii >>>   http://amvcaawards.dstv.com/ au www.amstel-nigeria.com

Baadhi ya vipengele vingine vinavyowaniwa ni

BEST ACTRESS IN A DRAMA

Stephanie Wilson – Living Funeral (3A)
Veronica Waceke – Higher Learning (3B)
Nse Ikpe-Etim – Journey To Self (3C)
Nkiru Sylvanus…

View original post 195 more words

D’BANJ NA G.O.O.D MUSIC KUNANI TENA???


larrybway91

D'banj Kanye 2 Imeonekana kama vile kuna mambo yanaendelea chini kwa chini ingawa bado haijaweza kudhibitishwa na wahusika wenyewe ambao ni  Msanii wa Nigeria, D’Banj ‘The Koko Master’ kuachana na rekodi label iliyomtambulisha kimataifa ya G.O.O.D Music tangu mwaka 2011 alivyoingia mkataba nayo iliyo chini ya Rapa Kanye West(Yeezy)…

Hiyo inatokana na ‘D’Banj’ kufuta jina la label iyo katika eneo la BIO kwenye akaunti yake ya Twitter na hivyo kuwapa watu maswali ya kwamba huenda staa huyo akawa ameshachukua hamsini zake. Unaweza ukatazama jinsi akaunti yake inavyoonekana kwa sasaa..

View original post

PNC ARUDI MIKONO NYUMA NA KUMWANGUKIA OSTAZ JUMA NA MUSOMA.


larrybway91

Staa wa kibao cha Imebuma,  Pancreas Ndaki ei kei ei PNC,  ametoa kali ya mwaka baada ya kurudi mikono nyuma na kumwangukia  bosi wa kampuni ya  Mtanashati Entertainment,  Ostaz Juma na Musoma na kumuomba amrudishe katika himaya yake.

 Awali PNC alidai kwamba ameamua kujitoa Mtanashati kutokana na management mbovu ,  hii sio mara ya kwanza kwa wasanii wa muziki waliowahi kufanya kazi na kampuni hiyo,  kuondoka na kisha kurudi wakiwa mikono nyuma kama ilivyomtokea Dogo janja hapo awali..

 ”hahaha jamani mziki ni kazi pnc arudi kuomba msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati” aliandika Ostaz kwenye akaunti yake ya Facebook kisha kupost picha na video iliyokuwa inamuonyesha PNC amempigia magoti kama inavyoonekana hapo chini.

View original post