PNC ARUDI MIKONO NYUMA NA KUMWANGUKIA OSTAZ JUMA NA MUSOMA.


larrybway91

Staa wa kibao cha Imebuma,  Pancreas Ndaki ei kei ei PNC,  ametoa kali ya mwaka baada ya kurudi mikono nyuma na kumwangukia  bosi wa kampuni ya  Mtanashati Entertainment,  Ostaz Juma na Musoma na kumuomba amrudishe katika himaya yake.

 Awali PNC alidai kwamba ameamua kujitoa Mtanashati kutokana na management mbovu ,  hii sio mara ya kwanza kwa wasanii wa muziki waliowahi kufanya kazi na kampuni hiyo,  kuondoka na kisha kurudi wakiwa mikono nyuma kama ilivyomtokea Dogo janja hapo awali..

 ”hahaha jamani mziki ni kazi pnc arudi kuomba msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati” aliandika Ostaz kwenye akaunti yake ya Facebook kisha kupost picha na video iliyokuwa inamuonyesha PNC amempigia magoti kama inavyoonekana hapo chini.

View original post