ROBBIN THICKE AKATISHA TAMASHA KUINUSURU NDOA YAKE.


larrybway91

Robin Thicke & Paula Patton Mwanamuziki wa Marekani Robbin Thicke  alilazimika kukatisha tamasha lake lililokuwa lifanyike katika mji wa Atlanta na kisha kukwea pipa kueleka nchini Canada kwa ajili ya mazungumzo ya kunusuru ndoa yake na aliyekuwa mkewe, muigizaji  paula Patton ambaye kwa wakati huo  alikuwa kwenye zoezi la uchukuaji wa filamu nchini humo.

Hata hivyo juhudi za Robbin hazikuweza kuzaa matunda licha ya mazungumzo ya muda mrefu na Paula ambaye alionekana kushikilia msimamo wake wa kuvunja ndoa kutokana na kuchoshwa  na kashfa za usaliti kila kukicha. Wawili hao walitangaza kuachana baada ya kudumu kwenye ndoa kwa takribani miaka 9 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume.

View original post

Advertisements