SNOOP DOGG AMALIZA BIFU NA BILIONEA OPRAH WINFREY IKIWA NI MARA YA KWANZA KUKUTANA.


larrybway91

Photo Supastaa Snoop Dogg wa Marekani ameweka kando tofauti zilizokuwepo kati yake na mtangazaji wa kipindi cha OWN, Bilionea Oprah Winfrey, walipokutana kwa mara ya kwanza kwenye pati ya Oscar na  kuamua kutokelezea  katika picha ya pamoja na baadae kuziposti kwenye akaunti zao za Instagram.

Wawili hao waliwahi kuingia kwenye vita ya maneno katika kipindi cha miaka ya 2007, huku sababu ikitajwa kuwa ni kitendo cha Oprah  kumchana laivu rapa huyo kupitia kipindi chake  kuwa na  chuki dhidi ya wanawake, kauli ambayo haikumpendeza Snoop ambaye alilalamika kwa kukosa  nafasi ya kujitetea na kusema kwamba hamkubali mama huyo hata chembe.

View original post