FAMOUS PROFILE:MAISHA YA MFALME HAILE SELASSIE.


image

Haile Selassie wa Ethiopia
Haile Selassie ( 23 Julai 1892 – 27
Agosti 1975 ) alikuwa Kaisari au
Negus Negeste wa Ethiopia .
Alizaliwa katika kijiji kiitwacho
Ejersa. Kabla ya kuwa mfalme aliitwa
Ras Tafari Makonnen. Jina lake la
kifalme lina maana ya “Utukufu wa
Utatu (Mtakatifu)”.

image

Pia anafahamika
kwa jina la Simba wa Yuda, Mfalme
wa wafalme (H.I.M).
Baba yake alikuwa mkabaila
Mwethiopia aliyeitwa Ras Makonnen
akawa gavana wa Harar , familia yake
ina watoto 11. Alikuwa Mkristo
muumini wa madhehebu ya
Orthodoksi ya Ethiopia.
Gavana wa mikoa
Ras Tafari Makonnen alikuwa bado
kijana alipopewa cheo cha gavana
wa Sidamo mwaka 1907. 1911
akarithi nafasi ya gavana wa Harar .
Wakati wa ugomvi kuhusu Negus
Mwislamu Lij Iyasu (1913-1916)
alisimama awali upande wa mfalme
lakini alifaidika zaidi na uasi
uliompindua Negus. Makabaila
waliomwondoa Iyasu mwaka 1916
walimteua shangazi yake aliyekuwa
binti wa Negus Negesti marehemu
Menelik II Zauditu kuwa malkia,
wakaamua pia Ras Tafari awe
mwangalizi wake.
Mtawala na Negus Negeste
Kwa njia hii Ras Tafari akawa
kiongozi muhimu zaidi nchini. 1928
Zauditu akampa cheo cha negus
chini yake mwenyewe. Baada ya kifo
cha Zauditu 1930 Ras Tafari
akapokea taji na cheo cha Negus
Negeste (au mfalme wa wafalme) wa
Ethiopia akajiita Haile Selassie.
Baada ya kupokea taji akafanya ziara
ya Ulaya.
Mwokozi wa Rastafari
Habari zake zikaenea kote duniani
zikasababisha kutokea kwa dini
mpya ya Rastafari iliyopokea jina
kutoka kwake, ingawa mwenyewe
alibaki mwamini wa Kanisa la
Orthodoksi, akiwa na daraja ya
shemasi . Watu weusi kisiwani
Jamaika, waliokuwa wajukuu wa
watumwa wa asili ya Afrika,
walisikia kwa mara ya kwanza ya
kwamba Mwafrika anaheshimiwa na
wafalme wa Ulaya, wakaona yeye ni
mwokozi wa Mungu aliyerudi duniani
kwa ajili ya watu weusi.
Haile Selassie alifukuzwa katika
Ethiopia mwaka 1936 Italia
ilipovamia Ethiopia, akarudi 1941
kwa msaada wa Uingereza
iliyoondoa Waiitalia nchini katika Vita
Kuu ya Pili ya Dunia .
Sifa na kasoro za utawala wake
Utawala wa Haile Selassie uliingizwa
Ethiopia katika Chama cha Mataifa
ikiwa nchi ya kwanza ya Afrika
kujiunga nacho. Baadaye ulimpa
nafasi kubwa katika harakati ya
uhuru wa Afrika na makao makuu ya
Umoja wa Afrika yalijengwa Addis
Ababa , mji mkuu wa Ethiopia.
Katika siasa yake ya ndani
alishindwa kuendeleza nchi yake
yake. Alikosa nguvu na nia ya
kumaliza utawala wa kikabaila
nchini uliosababisha umaskini mkali
kati ya wakulima waliopaswa
kuwaachia wakabaila sehemu ya
mazao.
Hivyo kimataifa Haile Selassie
aliheshimiwa sana lakini ndani ya
nchi maendeleo yalikwama
wanafunzi na wasomi wakikasirikia
na wakulima maskini walikufa njaa
mara kwa mara.
Mapinduzi ya 1974 na kifo
Njaa kubwa ya 1972–73 katika
majimbo ya Wollo na Tigray
ikafuatwa na mapinduzi ya kijeshi ya
1974. Kamati ya kijeshi ya Derg
ikamkamata tarehe 12 Septemba
1974.
Kifo chake kikatangazwa tarehe 28
Agosti 1975 na haieleweki kama
aliuawa au kama alikufa kutokana na
ugonjwa.
Baada ya kuondolewa kwa Derg
mabaki ya maiti ya Kaisari
yalipatikana mwaka 1992 chini ya
sakafu ya choo cha jumba la kifalme
alikokamatwa. Tarehe 5 Novemba
2000 mabaki hayo yalipewa mazishi
ya kifalme katika kanisa kuu la
Kiorthodoksi la Addis Ababa.
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa
Uhabeshi bado ni mbegu .

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements