CHIDDY BENZ KUANDAA CONCENT IITWAYO “GET TOGETHER PARTY ”


image

Chidi Benz amepanga kufanya tukio
kubwa kwenye muziki ambalo
halijawahi kufanyika Tanzania.
Rapper huyo anataka kuwakutanisha
wasanii wote wa Tanzania ambapo
wataongea na kubalishana mawazo
kuhusu muziki wa Tanzania, kula,
kunywa na kuburudika pamoja.
“Nahitaji watu wote tukusanyike,
tukutane kwa siku moja iwe kama get
together party,” Chidi ameiambia
Bongo5.
“Iwe kama concert lakini ya wasanii
tupu, wasanii wote then tuongee
kuhusu mipango, tuongee kuhusu
muziki wetu unaenda wapi, umetoka
wapi, wapi upo, kitu cha kufanyika
kwa baadaye, kitu cha kufanyika kwa
sasa hivi, kitu cha kufanyika kuokoa,
kutanua zaidi, kufungua zaidi,
kuupatia nafasi zaidi. Kwa wale
ambao wako juu, kwa wale ambao
wako chini, kwa wale ambao
wametoa single, kwa wale ambao
hawajatoa single. Ni miksa, kwa
wasanii wote ambao wanataka
kufanya muziki wetu wa Bongo Flava
pamoja na Hip Hop na kila tu,”
amesema Chidi.
Ameongeza kuwa party hiyo
itawahusisha pia hata wasanii wa
Tanzania wa nchi za nje ambapo
amepanga kuwaunganisha kwa njia
ya Skype na kwamba hadi sasa
wasanii wote aliowapigia na kuwapa
wazo hilo wamekubali kushiriki.
“Radio zote zitakuwepo, blog zote
zitakuwepo, vyombo vya habari vyote
vitakuwepo,” ameeleza Chidi na
kuongea kuwa wasanii wote wa kike
watahusika kwenye masuala ya
kupika kama wafanyavyo kwenye
familia na pia wanaume wakifanya
shughuli za kiume.
“Wa kiume watakuwa busy kubeba
makreti, soda nini, kuvunja kuni yaani
tunataka kufanya vitu kitamaduni
kama vile tunavyofanya nyumbani,
kama vile tunavyofanya kwenye
maharusi. Idea yangu nataka nione
wasichana wote, nione Lady Jaydee,
Ray C, Stara, Linah nani wamevaa
khanga na vitenge wanakatakata
vitu, wanapika, wanakaanga misosi.
Na Diamond, Ommy Dimpoz, Richie
Mavoko, Juma Nature, Mchizi Mox,
MB Dogg nani kwa pamoja
wanaenda kubeba makreti nini
kuweka ndani, kusafisha, kupiga deki
ukumbi kama nini, yaani
kinyumbani.”
Amesema pia kutakuwepo na
burudani mbalimbali ambapo
wasanii watajitolea kuwaburudisha
wenzao na kuongeza kuwa
ameshaongea na wasanii wengi huku
wengine akiendelea kuwapa taarifa.
“Naendelea kuongea na wengine,
naendelea kuwapigia simu wengine
kuwafahamisha. Mpaka wote
watakaposema sawa tuandae, tujue
wapi tutafanyia, ukumbi gani
tutafanyia na siku gani na kazi
iende.”
Chidi amesema kuna imani mitaani
kuwa yeye ni mtu mgomvi lakini huo
si ukweli na kila msanii anafahamu
kuwa yeye ni mtu wa watu na ndio
maana ameamua kufanya mradi huo.
“Nachohitaji kiwekwe wazi ni
kwamba sio kila point lazima watu
waweke negative. Sio kila mtu
akiongea kitu, watu waweke negative
‘Chidi anatafuta kiki tu, labda kaona
yupo kimya’ hapana, vitu vingine ni
positive. So nahitaji ushirikiano wa
vyombo vya habari kuwasambazia
watu na kuwafikishia watu habari na
tuombe Mungu hiyo siku itokee na
ifanyike.”

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements