Mtandao Mpya wa Mawasiliano ya SIMU za mkononi waanzishwa Leo jijini Daresalaam uitwao Smart Telecom.


Mtandao mpya wa mawasiliano ya
simu ‘Smart Telecom’ umezinduliwa
leo jijini Dar es salaam katika Hotel
ya Serena ambapo msanii wa
vichekesho nchini Hemed Maliyaga
maarufu kwa jina la Mkwere
amechukua nafasi ya ubalozi hapa
nchini.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart
East Africa, abellatif bouzian
akizungumza
Akizungumza na waandishi wa
habari, Mtendaji mkuu wa Smart
Telecom, Abdellatif Bouziani
amesema mtandao huo ulipewa jina
na Wanaafrika Mashariki baada ya
kuandaa mchakato wa uliyoitwa
‘Give us a Name’
“The name Smart was chosen as the
name by the people of East Africa in
an innovative naming campaign,
‘Give us a Name’, Smart Telecom is
under Industrial Promotion Services
(IPS) Kenya, a subsidiary of the Aga
Khan Fund for Economic
Development (AKFED),”alisema
Abdellatif Bouziani
Bouziani alisema mtandao wa Smart
Mobile umeanza na unatoa huduma
hapa nchini kwa kiwango cha chini
ambacho kinalingana maisha ya
Mtanzania mwenye maisha ya
kawaida

image

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart
East Africa, Abellatif Bouzian
(kushoto) na katikati ni Hemed
Maliyaga aka Mkwere ambae ni
balozi wa Smart Telecom wakiwa na
mdau wao
Katika hatua nyingine balozi wa
mtandao huo hapa nchini
mchekeshaji, Mkwere amesema
mtandao huo utawawezesha
wananchi kuwasiliana kwa bei ya
chini kulingana na maisha halisi.
“Kwanza leo nimefurahi kukutana na
mabosi wangu na pia napenda
kuwaambia Watanzania wenzangu
wajiunge na mtandao wa Smart
Telecom ambao una huduma za chini
kulingana na kipato cha Mtanzania.
Kwahiyo mimi kama balozi wenu
nimefurahia kuona kuna mtandao
ulioanzishwa kwaajili ya kuhudumia
watu wetu.”

image

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart
East Africa, Abellatif Abouzian
akimkabidhi mdau zawadi

Posted from WordPress for Android,by hailedavy