MTAZAME “Lameck Ditto akiongelea kampuni yake, ukulima na sababu za ukimya” on YouTube


image

Unaweza ukawa hujamsikia Lameck
Ditto kwa muda mrefu, lakini
muimbaji huyo wa THT anaendelea
kufanya mambo makubwa. Kwa sasa
akishirikiana na Amini, wanamiliki
kampuni ya masuala ya ubunifu na
matangazo ambayo inafanya kazi na
makampuni makubwa nchini.
“Hata nisiposikika sauti yangu
kwenye redio, vipo vitu vingine chini
ambavyo naendelea navyo lakini
ndani ya muziki humo humo,” Ditto
ameiambia Bongo5. “Ninayo
kampuni ambayo tunashare mimi na
Amini, Greenlight Music, inafanya
matangazo mengi sana mimi nakuwa
nyuma kule, nafanya ubunifu tofauti
tofauti, nafanya voice-over nyingi
sana, vipindi vingi katika TV
zinasikika, lakini hata matangazo
mengine makubwa tu yanahithit, zote
ni kazi ambazo nazifanya.”
Ditto amesema kuna watu
waliogundua kipaji chake cha ubunifu
tofauti na kuimba tu na akaamua
kuchukua kama changamoto na
kuifanyia kazi kwa takriban mwaka
mmoja na ndipo alipoamua
kuanzisha kampuni.
Katika hatua nyingine, Ditto
amesema kwa sasa ameamua
kuwekeza kwenye kilimo na sasa
anamiliki shamba la ekali 16
wilayani Bagamoyo ambako analima
mananasi. “Mimi napenda kilimo
ndio maana nimeamua kuwekeza
huko, ukiacha tu kukipenda na
kuinvest, kilimo ni kitu kinacholipa
sana kwasababu uwekezaji wake sio
mkubwa sana, ni kitu ambacho kila
mtu anaweza kufanya,”amesema.
Kuhusu ukimya wake, Ditto amesema
si wa bahati mbaya kwakuwa muziki
ni kitu anachokipenda kuliko kitu
chochote.
“Ni kitu ambacho mimi nimepanga,
lakini pia nina utaratibu wa namna
ambavyo mimi nyimbo zangu
ninazitoa. Pamoja na hivi
unavyoniona lakini mimi ni mmoja
wa wasanii wenye nyimbo chache
sana. Ukiacha dunia ina mambo
ambayo nilifanya na Afande Sele,
nina nyimbo mbili tu nyingine,
Tushukuru Kwa Yote na Wapo lakini
miaka 10 sasa, unaniskia,
tunakutana.”
Ditto amesema ataachia wimbo wake
mpya hivi karibuni.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements