Young Killer Asema anataka Aitwe.” #MSODOKI “.UNATAKA JUA SABABU? IJUE HAPA –>


image

Rapper wa ‘Mrs Superstar’ kutoka jiji
la Miamba mwanza anataka kuanzia
sasa aitwe MSODOKI na sio Young
Killer tena kutokana na sababu moja
kubwa.
Inawezekana umeshamskia sana
Young Killer akitaja MSODOKI katika
nyimbo zake, na pia analitumia
katika mitandao ya kijamii, rapper
huyo ameelezea lilipotoka jina hilo
na sababu kubwa ya kutaka aitwe
Msodoki badala ya Young Killer.
“Msodoki ni jina la familia yangu,
familia yangu ndio inaitwa Msodoki,
pia kipindi naanza kuitwa Young
Killer nilikuwa under 18, saizi
napenda sana kuitwa Msodoki
kwasababu nishavuka sasa hivi nina
miaka ishirini Ndio maana naliweka
sana msodoki mbele”.Amesema
Young Killer Msodoki kupitia XXL ya
Clouds FM.
Msodoki leo ametambulisha single
yake mpya ‘My Power’
iliyotengenezwa katika studio ya
Classic Sound.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements