BAADA YA MAAMUZI YA DOGO JANJA KUAMUA KUREJEA TIPTOP CONNECTION HAYA NDIO MANENO YA BABA YAKE:


image

Alhamisi ya March 20 2014 lilitoka
tamko ambalo lina maamuzi ya
msanii wa bongofleva Dogo Janja
kuhusu kuomba msamaha na kuhitaji
kurudi kwenye kundi lake za zamani
la Tiptop connection na kuyasahau
yaliyopita kati yake na aliyekuwa
meneja wake pia ambae ni Madee.
Stori hii ina pande nyingi sana
ambazo zitazungumza kupitia
hapahapa millardayo.com na AyoTV
l akini kwa kuanzia, baba mzazi wa
Dogo Janja amepata nafasi
kuzungumza kwa mara ya kwanza
baada ya mtoto wake kuomba
msamaha.
Anasema >>’ Dogo Janja alishakua
mtu mzima na tayari nilishawahi
kumwambia achague mahali
atakapoona kuna manufaa kwake,
a kishafanya maamuzi yake huwa
ananishirikisha kwenye kujadiliana,
tayari alishawahi kuniambia kuwa
atafanya maamuzi baada ya kuona
Mtanashati hakuna muelekeo
wowote na hakuna anachopata ndipo
akaniambia baba mimi mtu yoyote
au kundi lolote nitakalokubaliana
nalo basi nitafanya nao kazi’.
Hayo ni maelezo ya Baba mzazi wa
Dogo Janja ambae ametoa baraka
zote kwa Janja kurudi kujiunga na
Tiptop Connection hivyo kazi imebaki
kusikia kutoka upande wa Tiptop
kufahamu kama wameukubali
msamaha wa Dogo Janja.
Source: TZA

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements