MABESTE AFUNGUKA JUU YA ISSUE YA B-HITS NA M-RAP LION


image

Mabeste, M-Rap na Pancho.
HIT MAKER wa kibao cha Sirudi
Tena, mabeste Venance amemtetea
msanii mwenzake, M-Rap kwa kudai
kusikitishwa na kitendo cha uongozi
wa Bhits kudai kuibiwa mistari ya
nyimbo ya usiende mbali aliyofanya
rapa huyo katika studio za AM
records.
Alienda mbele zaidi kwa kusema
kama ishu ni kukopi na kupesti,
mbona hata yeye kipindi yupo Bhits,
mdundo wa nyimbo yake ya sirudi
tena ulinakiliwa na producer Pancho
katika ngoma ya Champion
aliyofanya Cheap Monkey na Chris
Brown!
Akifunguka LIVE bila ya kupepesa
macho, Mabeste aliandika hivi
kwenye ukurasa wake wa Facebook,

”Nasikitika Pancho Latino na
Uongozi wa Bhits kwa
kulalamika kua M-Rap
ametumia mistari yao katika
Track yake aliyoifanya Am
Records (usiende mbali) kuwa
ametumia Verse alizowahi
kuandika kipindi yuko Bhits na
kuamua kutoa hiyo Track
yenye hiyo Verse ambayo ni
(only you remix)… sasa mbona
(only you remix) waliyoitoa
Bhits ile chorus aliyoifanya Jux
niliandika mimi wakat niko
Bhits!! Je mbona wao
wametumia mistari yangu
wakati mimi siko Bhits? Na
kama issue ni Copy n Paste au
kuishiwa na idea,mbona beat
iliyotumika kwenye Track
yangu ya “SIRUDI TENA”
Pancho amei Copy kwenye
Track ya (cheap monkey ft
chriss brown – champion)?? Je
ni haki wanachofanya??
Ama wanataka kumuaibisha
tuu dogo(M-rap), mbona wao
pia wanazingua nao???
#MabesteArmy !”

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements