OPRAH WINFREY Anzisha Mradi wa Majani Ya Chai Uitwao “OPRAH CHAI ”


Malkia wa talk show Oprah Winfrey
ameingia katika biashara mpya ya
majani ya chai ambayo ameyaita jina
la Kiswahili ‘Oprah Chai’.

image

Oprah Winfrey na Howard Schultz
Oprah ameungana na rafiki yake
bilionea Howard Schultz wa kampuni
ya Starbucks katika kuanzisha mradi
huo wa majani ya chai, ambao
umetangazwa Jumatano ya wiki hii
wakati wa mkutano wa kila mwaka
wa kampuni hiyo.

image

Majani hayo ya ‘Oprah Chai’
yatapatikana katika ladha
mbalimbali ikiwemo ya mdalasini,
tangawizi, iliki pamoja na karafuu.
Katika kila bidhaa ya ‘Oprah Chai’
itakayouzwa, kampuni iliyoingia ubia
na Oprah ya Starbucks itatoa
mchango kwa shule ya wasichana
iitwayo ‘Oprah Winfrey Leadership
Academy’ iliyoianzishwa na
inayofadhiliwa na Oprah, iliyoko
nchini Afrika Kusini.
Oprah Chai itaingia sokoni (April 29)
huko Marekani na Canada.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy