SPRITE WATENGENEZA KINYWAJI CHENYR JINA LA LEBRON JAMES KAMA BRAND


image

Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu
nchini Marekani, Lebron james
anayechezea Miami Heat,
ameendelea kuwapa STRESS mastaa
wenzake kutokana na mikataba
minono anayoipata kutoka katika
makampuni mbalimbali makubwa
ikiwemo kampuni ya Nike
iliyomtengenezea raba aina ya
Lebron james 11, kampuni ya
Samsung pamoja na gums zake,
hivyo kumfanya aweke kibindoni
mkwanja mrefu sana.
Katika kudhihirisha kuwa hakupata
bure tuzo ya mchezaji bora Duniani
wa kikapu mwaka 2013-14, kampuni
ya Sprite imeingia nae mkataba kwa
kutengeneza kinywaji cha ‘Sprite 6
Mix by Lebron James’
kitakachokuwa na ladha tatu tofauti
anazozipenda yani limao, tunda
damu na chungwa . Kinywaji hicho
kitaanza kusambazwa rasmi nchini
humo kwa muda maalum kikiwa
kwenye chupa yenye ujazo wa mililita
30 / 19.2ounce.
”Sijawahi kufikiri kama ningekuwa
na ladha yangu mwenyewe siku
moja, alisema Lebron katika taarifa
aliyokuwa akiitoa. ”Nilikuwa na
wakati mkubwa wa kufanya kazi na
timu ya Sprite ya kuweka ladha
nizipendazo katika moja ya bidhaa
nizipendazo. Najivunia kwa hilo na
ningependa mashabiki wangu
wajaribu waone ladha yake”.

image

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements