TWIGA AAGA MWILI WA MAREHEMU KWA KUTOA BUSU KAMA SALAMU ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA ZOO


image

Twiga akitoa salamu za mwisho kwa
kumbusu Mario aliyelala kwenye
kitanda.
Tukio hili linaweza kuwa ni geni kwa
baadhi ya watu ila ukweli ni
kwamba, Wanyama nao
wanaufahamu kama wa binadamu
ingawa sio kwa kiwango kikubwa,
hiyo inatokana na aliyekuwa
mtunzaji wa wanyama katika zoo ya
Diergaarde Blijdorp iliyopo katika mji
wa Rotterdam nchini uholanzi kwa
kuagwa na wanyama aliokuwa
akiwahudumia lkwenye kituo hicho
kwa muda mrefu kabla ya kuugua
maradhi ya ugonjwa wa kansa
yaliyomfanya apooze na kuwa mtu
wa kulala kitandani muda wote.
Mario mwenye umri wa miaka 54
alipata nafasi ya kuagwa na
wanyama baada ya kuiagiza
hospitali aliyokuwa akipatiwa
matibabu kumpeleka akiwa kwenye
kitanda ili aweze kuaga kabla ya
mauti kumkuta, katika hali ya
kushangaza, mnyama jamii ya Twiga
alionyesha upendo wa hali ya juu
kwa kumbusu mfanyakazi huyo ikiwa
kama ishara ya kuagana nae.

image

Posted from WordPress for Android,by hailedavy