VIDEO:”Raia Wawili wa Nigeria Wakamatwa na ‘Cocaine.'” on YouTube


TAZAMA VIDEO::NJIA MPYA YA
USAFIRISHAJI WA MADAWA YA
KULEVYA ILIYOGUNDULIWA BAADA
YA KUWANASA WANAIGERIA NA
MTANZANIA MMOJA
RAIA watatu wa Nigeria na
mwanamke wa Kitanzania
wamekamatwa na polisi jijini Dar es
Salaam, wakituhumiwa kujaribu
kusafirisha madawa ya kulevya
kwenda nchini Liberia. Watuhumiwa
hao wanadaiwa kuwa walikuwa
mbioni kutuma mihadarahi hiyo,
ikiwa kwenye vitabu, kwa kutumia
Wakala wa Usafirishaji Mizigo ya
DHL.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu
Dar es Salam, Suleiman Kova alitaja
majina ya Wanaijeria hao kuwa ni
Sunday Chaidikaobi (42), Chukwuma
Favour (31), na Franklin Indubuisi
(41). Mtanzania aliyebambwa
pamoja na Wanaijeria hao ametajwa
kuwa ni bi Hadija Ngoma (43), mkazi
wa Kimara Temboni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, polisi
walipata taarifa juzi, Machi 18, kuwa
kuna watu wanne wanajihusisha na
usafirishaji wa dawa za kulevya
waliokuwa katika ofisi za DHL
zilizopo Barabara ya Sam Nujoma.
Kufuatia taarifa hizo, Kamanda Kova
amesema “makachero walifuatilia
suala hilo na hatimaye siku hiyo saa
8:30 mchana watu hao walikamatwa
wakiwa na kifurushi wakijiandaa
kukisafirisha kwenda nchini Liberia.”
Alisema polisi walipopekua kifurushi
hicho, walikuta vitabu vitatu vya
Kiingereza. Walipopekua vitabu hivyo,
walikuta madawa aina ya heroin
katika kurasa za mwanzo.
“Katika vile vitabu kurasa ya kwanza
inayofunika lile jalada gumu kwa
ndani, walikuwa wamefunua na
kuweka unga huo na katika ukurasa
wa nyuma vivyo hivyo kwa vitabu
vyote,”aliongeza.
Unga huo unaokadiriwa kuwa na
uzito wa nusu kilo, umepelekwa kwa
mkemia mkuu wa serikali kwa
uchunguzi zaidi kubaini thamani na
uthibitisho wa madawa hayo. H/T
HabariLeo Inaonekana Wanigeria
wanakuja kwa kasi kwenye biashara
hii ndani ya Afrika Mashariki. Miezi
kadhaa iliyopita, Wanigeria wawili
walikamatwa katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Jomo
Kenyatta nchini Kenya, wakijaribu
kusafirisha dawa za kulevya aina ya
cocaine zenye thamani ya takriban
shilingi milioni 120; kama
inavyoonesha video hii hapa

image

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements