ALICHOSEMA NAZIZ.KUHUSU NDOA YAKE KATIKA INTERVIEW NA KITUO CHA NTV “#theTrend: Nazizi, the original Kenyan girl returns” on YouTube


Rapper wa kundi la Necessary Noize
la Kenya, Nazizi amekanusha
shutuma kuwa aliachana na mume
wake wa miaka mitano ili avune mali
walizokuwa wanamiliki.
Akiongea kwenye kipindi cha The
Trend cha NTV ya Kenya jana, Nazizi
alidai kuwa kwanza mume wake
huyo kutoka Tanzania si tajiri wa
Mombasa kama baadhi ya watu
wanavyodai.
Alisema kuwa waliachana kwa
sababu waligundua kuwa hawakuwa
na muda wa kutosha kuwa pamoja
kwakuwa mara nyingi walikuwa ni
watu wa kusafiri na kwasababu wote
wanampenda mtoto wao wa kiume
walilazimika kuokoa ndoa yao japo
ilifika sehemu wakaona haiwezekani.
Wawili hao walinununua kiwanja
pembezoni na bahari huko Lamu
nchini Kenya na alidai kuwa taraka
yao ya kiislamu ambayo imetoka
tayari haitahusisha masuala ya
kugawana mali.
“Hakuna anayepata chochote, hapati
changu, nami sipati chake chochote,
tulichokuwa tunataka wote ni mtoto
wetu awe na maisha mazuri” alisema
Nazizi.
“Kama ningekuwa nimeolewa na
mwanaume tajiri nisingeomba
taraka… hapana, natania tu.. lakini
sio kweli.”
Rapper huyo pia jana alitambulisha
wimbo wake mpya 254 (Born and
Raised in Nai) ambao ni wa kwanza
kutoka kwenye album yake mpya
‘Evolussion’.

image

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements