ASILIMIA KUBWA YA WASANII WALIOJITOA TIPTOP CONNECTION MAMBO YAO HAYAWANYOKEI JE BUT KWANINI?


Wako wapi MB Dog, Z-Anto, Keisha,
Pingu, Spark, Dongo Janja na
wengine waliowahi kujitoa Tip Top
Connection? Kuna nini Tip Top,
kwamba ukijiondoa tu huwezi
kufanikiwa mbeleni? Kwanini ni
wasanii wachache tu, tena anaweza
kuwa Cassim Mganga peke yake
ambaye baada ya kujiondoa kwenye
himaya hiyo yenye makazi yake
Manzese jijini Dar es Salaam,
amefanikiwa kuwa na career ya
kueleweka? Wengine wote, wamefeli..
big time.

image

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa wengi
wakiondoka hutoa maneno ya kashfa
na hivyo kujikuta wakinyea kambi.
Hebu tuwaangalia hawa watatu,
Dogo Janja, Z-Anto na MB Dog
Dogo Janja
Unakumbuka June 2012, kipindi Dogo
Janja ameondoka Tip Top? Habari
hiyo ilikuwa kubwa kiasi ambacho
simu za Madee na Dogo Janja
zilikuwa busy kwa interview. Kila
pande ilikuwa ikiutupia lawama
upande wa pili.
Kama umesahau wacha
tukukumbushe ilivyokuwa.
Sababu zilizotajwa na Tip Top
Connection ni kwamba Dogo Janja
alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.
Kwa mujibu wa interview aliyofanya
na Bongo5, uonevu na dhuluma
ndivyo vilivyomchosha Dogo Janja
kuishi Dar es Salaam na kujiondoa
kwenye himaya hiyo.
Alisema tangu aje Dar es Salaam
hakuwahi kusaidiwa chochote na
Madee zaidi ya mambo ya muziki
pekee huku kula, malazi na ada ya
shule vikifanywa na rafiki yake
Madee aitwaye Abdallah Doka
ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi
kwake.
Alisema kutokana na ngoma zake
kujipatia umaarufu alikuwa akipata
show nyingi nchini na zote alikuwa
halipwi chini ya milioni moja.
Kilichokuwa kinamsikitisha anasema
ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki
mbili na hivyo kumfanya aishi kwa
tabu licha ya kuingiza hela nyingi za
show. “Nilikuwa navumilia tu bro
kwasababu kila nilipolalamika
kuhusu mambo ya hela Madee
alikuwa mkali sana,” aliiambia
Bongo5.
Dogo alidai ilikuwa inafikia wakati
akifanya show za ukumbuni hulipwa
elfu hamsini au chini ya hapo na
wakati mwingine alikuwa halipwi
kabisa. Alisema tamaa ilizidi
kumwingia Madee kiasi cha
kumnyang’anya kadi yake ya benki
na kuanza kuchukua hela bila kujua
password aliipata wapi. “Kuna
wakati nilikuwa nataka kumtumia
mama laki moja, Madee akanikataza
eti kwakuwa watadhani nina hela
sana,” alisema.
Aliongeza kuwa kuna siku Madee
alimpigia simu na kumwambia kuwa
kaka yake wa Kibaha ameandaa
show ya CCM na angemlipa shilingi
laki moja. “Hivi kweli bro mimi ni mtu
wa kufanya show ya laki moja?”
alihoji. Hata hivyo aliamua kukubali
ili kuepusha lawama.
Baada ya show kumalizika alisema
yeye na back up artist wake
walirudishwa saa saba usiku wakati
asubuhi yake alitakiwa kwenda
shuleni kuchukua namba ya mtihani
na kuandaa dawati la kukalia. Dogo
Janja alisema kuwa ilimuuma sana
kwakuwa muziki haujampa chochote
licha ya Madee ambaye huwa hapati
hata show kumtumia kimaslahi na
hadi kufikia hatua ya kujenga nyumba
yake.
“Ni kama vile Madee alinipanda ili
anivune,” alisema.
Alifunguka kuwa hadi kufikia Tip Top
watangaze kumfukuza alikuwa kwa
Tundaman akipiga story na Madee
akamuita kisha kuanza kumpiga na
kwamba alichukua simu yake
akaondoka nayo. “Jamaa alianza
kujitumia meseji kutoka kwenye simu
yangu kwenda kwake za matusi ama
kuwa nataka kumroga. Jana
nimemuonesha Milard hizo meseji na
amesikitika sana.”
Alisema kitendo cha kumwambia
Madee kuwa amechoka na anataka
kurudi nyumbani ndicho kilimfanya
amfanyie yote hayo hadi kumwambia
kuwa watahakikisha wanambania
asifanye vizuri tena kwenye muziki.
Pia amedai kuwa Madee aliwapigia
simu wazazi wake ili wamkataze
Dogo Janja asifanye interview na
vyombo vya habari.
“Wanajua nikiongea wataabika sana.”
Baada ya drama zote hizo ndipo
Ostaz Juma akaingia kwenye picha.
Alimtumia nauli ya ndege rapper
huyo kutoka Arusha kurejea Dar na
akajiunga na Mtanashati
Entertainment ambayo wakati huo
ilikuwa na heshima kidogo. Dogo
Janja alipewa maisha, akalipiwa ada
ya shule na kutoa ngoma iitwayo Ya
Moyoni aliyomshirikisha PNC.
Haikupita muda, mambo yakaanza
kutokota.
Kwa mara nyingi Ostaz Juma
alimfukuza na kumrejesha tena
rapper huyo kwa madai kuwa hakuwa
na nidhamu. Hata hivyo, imefika
wakati ambapo Mtanashati
Entertainment imekosa muelekeo na
Dogo Janja anahisi meli inazama.
Kuomba msamaha ili mambo yaende
ni kitu kisichoepukika kwake
kwakuwa ni kweli Dogo Janja wa
‘Mtoto wa Uswazi’ ft Godzilla
amepotea kabisa.
Z-Anto
Ni ngumu kuamini ukubwa wa Z-
Anto baada ya kutoa hit single yake
‘Binti Kiziwi’ ungekuja kuyeyuka
kama barafu ikutanapo na jua kali.
Enzi Binti Kiziwi inahit, hakuna
msanii aliyekuwa na show nyingi
kama Z-Anto. Hata hivyo, meneja wa
Tip Top Connection aliwahi kudai
kuwa kipindi hiki ndipo msanii huyo
alianza kuota ‘majipu’ kwapani na
kuanza pozi nyingi. Jambo hilo
lilimkera Babu Tale kiasi cha kuamua
kuifuta kabisa video mpya ya msanii
huyo iliyokuwa inategemewa
kumpeleka juu zaidi. Baada ya
kuondoka Tip Top mpaka leo hii, Z-
Anto si yule tena wa zamani na
ukweli hali yake kimuziki ni mbaya.
“Nililazimika kushuka kwa sababu
hiyo. Lakini nilipokuja kuzigundua
zile njia nikaweza kupenya na ngoma
binafsi nilijisimamia mwenyewe kwa
kila kitu ambayo ndio hiyo Kisiwa
cha Malavidavi,” Z-Anto alikiambia
kipindi cha Mseto cha Radio Citizen
ya Kenya hivi karibuni japo alidai
kuwa hadi leo Babu Tale anamtaka
arejee kundini.
“Mpaka kesho (Babu Tale) bado
ananipenda. Hata ukimuuliza katika
wasanii wake anaowapenda atatajwa
wawili asishindwe kunitaja mimi.”
MB Dogg
Unazikumbuza Latifa na Si
Uliniambia? Hizo ni miongoni mwa
nyimbo bora za Bongo Flava za muda
wote lakini yuko wapi MB Dogg?
Kama ilivyokuwa kwa Z-Anto, naye
baada ya kujitoa Tip Top, mambo
yalienda mrama. Ilimchukua miaka
mingi MB Dogg kuweka ‘ego’
pembeni na kukubali kuwa kweli
amepotea na anaiihitaji Tip Top kiasi
cha mwaka huu kuweka mambo
sawa na Babutale.
“Lakini kwa sasa nataka tumuangalie
Mb Dogg kwa macho mawili,” Tale
aliiambia Millaayo.com hivi karibuni.
Mb Dogg ana kipaji watu wanaujua
uwezo wa Mb Dogg, Mb Dogg sio
kama amepotea hapana ila hana
uongozi anahitaji promo ya nguvu tu
akipata hiyo anarudi kupiga hela
kama zamani.”
Hata yeye mwenyewe MB hivi
karibuni alikiri kuwa kufanya muziki
bila kuwa na uongozi wa
kukusimamia ni kazi bure.
“Tip Top nilitoka na ndio kitu
ambacho kilinirudisha nyuma sana,”
MB Dogg aliiambia Bongo5 March 17
mwaka huu.
“Pale nilikuwa nafanyiwa kila kitu,
nilikuwa narekodi tu kazi yangu vitu
vingine vyote wanafanya wao so
baada ya kutoka na kujisimamia
mwenyewe nikaanza kuyumba na
kuhangaika huku na kule. Kwahiyo
kitu ambacho nimegundua msanii
bila management nzuri huwezi fika
mbali asikwambie mtu. Msanii
anahitaji kuongozwa, kushauriwa na
mambo mengine. Sasa hivi nipo Tip
Top tumeingia makubaliano mapya
ya kazi ndio maana nashukuru
Mungu ngoma yetu mpya ‘Umenuna’
inasonga kidogo kidogo mpaka
kieleweke.”
Kinachowaumiza zaidi wasanii
walioondoka Tip Top ni kwamba
wasanii waliosalia mathalani Madee,
wameendelea kufanikiwa zaidi.
Mwaka jana pekee, Madee anadai
kuingiza zaidi ya shilingi milioni 150
kwa single yake moja tu ‘Sio Mimi’.
Meneja wa Tip Top, Babu Tale
akishirikiana na Said Fela ndio walio
nyuma ya mafanikio ya Diamond
Platnumz, kwahiyo ni wazi kuwa
Babu Tale ni ‘hot cake’ kwa sasa na
ndio maana wasanii wa Tip Top
waliojiondoa wako radhi kumuomba
msamaha ili warejee kundini.
Swali ninalokuacha nalo msomaji ni
Je! Haiwezekani msanii aliyejiondoa
Tip Top kuwa na career yenye
mafanikio?

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements