AU KUZIDISHA VITA DHIDI YA AL-SHABAB


Al Shabaab

image

Mamia ya wanajeshi wa Muungano
wa Afrika wanaukaribia mji muhimu
wa Koryoley, ulio umbali wa kilomita
90 Kusini Magharibi mwa mji mkuu
Mogadishu.
Mji wa Koryoley, umekuwa chini ya
udhibiti wa kundi la wanamgambo la
Al Shabaab kwa miaka mitano
iliyopita.
Mwandishi wa BBC aliye katika eneo
hilo anasema kuwa wanajeshi hao
wako umbali wa kilomita 10 kutoka
mjini humo.
Anasema kuwa ikiwa wanajeshi hao
wataukomba mji huo, utakuwa
ukombozi wao mkubwa wa mji tangu
kuanza harakati hizo dhidi ya Al
Shabaab mwezi Machi mwaka jana
wakiungwa mkono na Umoja wa
Mataifa.
Wanajeshi hao wamefanikiwa
kukomboa miji mingine muhimu na
hata kuwatimua wapiganaji hao
kutoka katika ngome zao kubwa.
Wengi wa wanajeshi wa AU ni kutoka
Uganda, wakisaidiwa na wanajeshi
wa Kenya, Burundi na sasa Ethiopia
pamoja na wanajeshi wa Somalia.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy