CHINA YAANZA KUCHUNGUZA PICHA MPYA ZA SATELLITE KAMA ZINA UHUSIANO NA NDEGE ILIYO POTEA


image

China imeanza kuchunguza picha
mpya za setilite zinazoonyesha kitu
kama mabaki ya ndege kwenye eneo
la kusini mwa bahari ya Hindi.
Picha hizo ni muhimu kwa ndege ya
Malaysia MH370 iliyopotea, maafisa
wa Malaysia wanasema.
Kaimu Waziri wa Usafirishaji
Hishammuddin Hussein amesoma
taarifa hiyo baada ya kukabidhiwa
ambapo amesema kuna kitu kama
mabaki ya ndege chenye ukubwa wa
mita 30 kwa 22 kilichoonekana.
Amesema serikali ya China
itaendelea kutoa taarifa zaidi hapo
baadae.
Ndege MH370 mali ya Shirika la
ndege la Malaysia ilipotea kwenye
masiliano ilipokuwa imeondoka
kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing
march 8 ikiwa na abiria 239.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements