DIAMOND KUANZA HARAKATI ZA KUVUKA BORDER SASA KUTAKA KUFANYA TRACK NA WA GHANA & WA NAIJA:


Ni ukweli usiopingika kuwa msanii
Diamond Platnumz ameendelea
kupata mafanikio makubwa
kimataifa kupitia hit single yake ya
mwaka jana ‘Number 1′ amabayo
alikuja kumshirikisha star wa Nigeria
Davido katika remix ya wimbo huo.

image

Licha ya video ya ‘Number 1 Remix’
kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza
katika Top 10 ya kituo kikubwa cha
TV cha kimataifa Trace Urban ya
Ufaransa, Diamond amesema kwa
sasa amekuwa akipokea maombi
kutoka kwa wasanii wa Ghana na
Nigeria wote wakitaka kufanya naye
Collabo, kitu ambacho zamani yeye
ndiye aliyekuwa akihangaika kutafuta
connection ya kufanya collabo na
wasanii wa huko.
“Ukiangalia saizi nyimbo inafanya
vizuri sana Nigeria inafanya vizuri
sana Ghana hapa nilipo nina collabo
kama tatu naombwa kutoka Ghana
watu wanaomba kufanya Collabo na
mimi, sio Ghana hadi Nigeria kuna
watu wanaoniomba mimi kufanya
nyimbo na mimi, wakati haikuwa
hivyo before…” Diamond aliiambia E
News ya EATV.
Ameongeza kuwa anatarajia kuachia
single mpya siku si nyingi ambayo
pia itakuwa ni moja ya collabo za
kimataifa ambazo amefanya na
wasanii mbalimbali. Pamoja na
kwamba hajaweka wazi ni wimbo
gani anaotarajia kuutoa, lakini
baadhi ya wasanii wakubwa ambao
ameshafanya nao collabo hadi sasa
ni pamoja na Iyanya na D’Banj wote
wa Nigeria.
Platnumz ameongeza kuwa mwisho
wa mwezi huu anatarajia kusafiri
kwenda tena Nigeria kushoot video
yake mpya pamoja na kufanya
collabo zingine kwaajili ya soko la
Afrika kwa ujumla.
“Tarehe 30 kama sikosei nasafiri
narudi tena Nigeria naenda kushoot
video yangu mpya, ukiacha tu video
kuna collabo collabo zangu naenda
kuzifanya za kiAfrika. Unajua kuna
vitu viwili kuna muziki wa East Afrika
na muziki wa Afrika kwa ujumla so
lazima uangalie market inafanyaje na
we ujue unafanyaje”. Alimaliza
Diamond.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy