HUU NDIO UKWELI KUHUSIANA 93•7FM DSM


image

Katika kile kinachoonekana ujio wa
redio mpya jijini Dar es Salaam,
uvumi umeanza kusambaa juu ya
kituo hicho kipya cha habari
ambacho jina lake bado
halijafahamika rasmi.

image

Fundi wa Ujerumani akijaribu
mitambo kwenye studio za kituo
hicho cha redio kilichopo Kawe, Dar
Kwa mujibu wa viashiria habari
mbalimbali na minong’ono
inayoendelea jijini Dar es Salaam,
masafa ya redio 93.7 FM DSM
yamekuwa gumzo katika viunga
mbalimbali ambapo watu wengi
wameingiwa shauku ya kutaka kujua
redio hiyo inaitwaje na watangazaji
wake ni akina nani!
Pamoja na kutojua kwa undani
maudhui kamili ambayo redio hiyo
itatumia katika vipindi vyake, kwa
mujibu wa utafiti wa haraka haraka
na wa chini chini tuliojaribu kuufanya
dalili zinaonyesha kuna mtazamo wa
kiburudani zaidi kwa namna moja
ama nyingine, kwa kuwa, baadhi ya
maswali ambayo ndiyo msingi wa
minong’ono ambayo watu wengi
wameyasoma kupitia akaunti ya
twitter ya masafa hayo @New937.
Baadhi ya maswali hayo yamekuwa
yakiwataka wananchi kuchagua
playlist za nyimbo wanazozitaka
ama kuzipenda na pia maswali
yanayohusu aina ya watangazaji
ambayo wananchi wanapendelea na
upepo kuegemea zaidi kwa wasanii
wa Bongo Flava Bongo Movie.
Inaeleweka mara nyingi kuwa redio
mpya mara nyingi huvutia baadhi ya
watangazaji, ma Dj, maprodyuza na
hapo ndipo swali la je kuna
uwezekano wa watangazaji na ma Dj
nguli ambao tunaweza kuwasikia
wakiibukia katika redio hiyo?
Tayari masafa hayo ya 93.7 FM DSM
yameshaanza kuteka hisia za wakazi
wa jiji la Dar baada ya picha na video
kadhaa za studio ambapo
matangazo ya redio hiyo yatakuwa
yakirushwa kuonekana kupitia
mtandao wa twitter na pia kwa
wahusika kuthibitisha uwekaji wa
nyimbo laki moja katika database ya
redio hiyo.
Moja ya wadau wa burudani na
sanaa ambaye tuna hisi anaweza
kuwa na uhusiano wa karibu kabisa
na umiliki ni Lady Jaydee ambaye
minong’ono inamzungumzia.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements