Maandamano Nchini Algeria kumpinga RAIS bouteflika


image

Rais Bouteflika
Maelfu ya raia wa upinzani nchini
Algeria wamehudhuria mkutano
mkubwa wa hadhara katika mji
mkuu wa Algiers ili kutaka watu
wasusie uchaguzi mkuu
utakaofanyika mwezi ujao.

Vyama vya upinzani vikiwemo vile
vya dini vimepinga harakati za rais
Abdelaziz Bouteflika kutaka
kuliongoza taifa hilo kwa muhula
mwingine wa miaka minne.
Wanasema kuwa hafai kuliongoza
taifa hilo baada ya ugonjwa wa
kupooza kumuathiri vibaya mwaka
uliopita.

Maandamano kumpinga Rais
Bouteflika
Mkutano huo ulifanyika ndani ya
ukumbi wa michezo ambapo watu
5000 walikusanyika wakilaani
harakati za Bouteflika kutaka
kugombea urais kwa muhula wa nne.
Wanataka mageuzi ya sheria pamoja
na kuishinikiza serikali kuangamiza
ufisadi.
Bwana Bouteflika ambaye ana umri
wa miaka 77 amekuwa haonekani
hadharani miezi ya hivi
karibuni,lakini waandishi wanasema
kuwa ushawishi alionao katika
chama tawala, jeshi na miongoni
mwa wafanyibiashara huenda
ukamsaidia kuchaguliwa kwa
muhula mwingine.
Amekuwa mamlakani tangu mwaka
1999 na alifutilia mbali sheria za
katiba mwaka 2008 ambazo
zilimruhusu tu kuwa mamlakani kwa
mihula miwili.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements