MAJESHI YA UMOJA WA AFRIKA.WAFANIKIWA KUTEKA MJI WA KORYOLEY ULIOPO NCHINI SOMALIA


image

Wanajeshi wa Muungano wa Afrika
wanameuteka mji muhimu wa
Koryoley, ulio umbali wa kilomita 90
Kusini Magharibi mwa mji mkuu
Mogadishu.
Mji wa Koryoley, umekuwa chini ya
udhibiti wa kundi la wanamgambo la
Al Shabaab kwa miaka mitano
iliyopita.
Mwandishi wa BBC aliye katika eneo
hilo anasema kulikuwa mlio wa
silaha na baadhi ya raia wa mji
wamekimbia.
Kutekwa kwa mji huo ni ukombozi
tangu kuanza harakati hizo dhidi ya
Al Shabaab mwezi Machi mwaka
jana wakiungwa mkono na Umoja wa
Mataifa.
Wanajeshi hao wamefanikiwa
kukomboa miji mingine muhimu na
hata kuwatimua wapiganaji hao
kutoka katika ngome zao kubwa.
Wengi wa wanajeshi wa AU ni kutoka
Uganda, wakisaidiwa na wanajeshi
wa Kenya, Burundi na sasa Ethiopia
pamoja na wanajeshi wa Somalia.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements