PAPA FRANCIS AWAASA KIKUNDI CHA ‘MAFIA ‘KUFANYA TOBA


image

Mkuu wa Mafia Italia Salvatore Riina:;
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
Papa Francis amewaonya
wanachama wa genge la Mafia
kwamba watakwenda motoni iwapo
hawatatubu dhambi zao.
Akizungumza katika sherehe ya
maombi ya ndugu na jamaa za
waathiriwa wa genge hilo waliouawa
nchini Italia,Papa Francis amesema
kuwa wanachama wa kundi hilo
hawawezi kutumia fedha
wanazopata kwenda peponi.
Wakati wa ibada hiyo majina ya watu
800 waliouawa na wanachama wa
genge hilo yalisomwa.
Waandishi wanasema kuwa lengo la
ibada hiyo ilikuwa kuonyesha
kwamba kanisa katoliki linapinga
uhalifu mbali na kujitenga na wakuu
wa genge hilo wanaodai kuwa
wafuasi wakubwa wa kanisa hilo.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements