KOMANDO BINTI (LADY JAYDEE ) ATOA BAADHI YA LYRICS ZA NGOMA YAKE MPYA IITWAYO “NASIMAMA ” KWA WASHABIKI ZAKE KAMA KIONJO CHA TRACK HIYO


image

Mwanamuziki wa kike nchini, Judith
Daines Wambura Mbibo(34) ‘Lady
JayDee’ amewaonjesha mashabiki
wake ‘chorus’ na ‘verse’ya kwanza
ya nyimbo yake mpya itakayotoka
hivi karibuni inayoitwa ‘NASIMAMA’ .
Staa huyo wa kibao cha Historia
anayesifika kwa kuwa na wafuasi
wengi kwenye mitandao ya kijamii,
aliachia kiitikio pamoja na verse ya
kwanza na kuwataka wale
wanaopenda kuimba nae wakae
tayari muda utakapofika..
Verse 1: Nasimama na Mola
Kwa kila jambo lile nitendalo
Maneno ya watu bakora
Yalinichapa nikaumia
Lakini machozi machozi nilolia
zamani yashafutika
Japo simanzi majonzi yalojaa
moyoni nikikumbuka
Nilishaambiwa zamani, kinyago
uchongacho hakikutishi ng’oo
Ndio maana nasimama, na
aliepanga
CHORUS: Aliepanga ni maanani,
shida na riziki zangu
Aliezitupa gizani, shida na tabu
zangu oooh x2

image

Posted from WordPress for Android,by hailedavy