Habari iliyo tikisa Dunia siku ya Leo na kuacha Simanzi kwa dunia “Malaysia PM Announces Flight MH370 CRASHES Into Indian Ocean – 24/03/2014 (Video)” on YouTube


image

Waziri mkuu wa Malaysia Najib
Razak
Shirika la ndege la Malaysia
limewaambia jamaa na familia za
abiria waliokuwa wanasafiri kwa
ndege iliyotoweka MH370 kwamba
ndege hiyo imepotea na kwamba
hakuna manusura.
Tangazo hilo limetolewa kwa familia
hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya
mkononi . Ndege ya Malaysia MH370
ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada
ya kuruka kutoka uwanja wa ndege
wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu
ikielekea Beijing.

image

Aidha tangazo hilo limekuja huku
juhudi za kutafuta mabaki ya ndege
hiyo Kusini mwa Bara Hindi
zikimalizika kwa siku ya tano bila
mafaniko.
Waziri mkuu wa Malaysia amesema
kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini
mwa Bahari Hindi, bila ya manusura
wowote.
Aliambia waandishi wa bahari kuwa
udadisi uliofanyiwa data ya Satelite
kutoka Uingereza ndio
umewathibitishia kwamba ndege
hiyo ilimalizia safari yake Magharibi
mwa mji wa Perth mbali na eneo
lolote la kutua.
Ameomba vyombo vya habari
kuheshimu familia za watu
waliokuwa ndani ya ndenge hiyo,
akisema kuwa anasikitishwa sana
kwani kipindi chote walichosubiri
taarifa njema , mwishowe imekuja
kuwa taarifa mbaya hata zaidi.
Ndege ya Malaysia MH-370,
ilipoteza mawasiliano wiki mbili
zilizopita na meli za nchi mbali mbali
pamoja na ndege zimekuwa
zikitafuta angalau mabaki ya ndege
hiyo bila ya kupata chochote.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements