Hukumu ya Kifo yatolewa kwa wafuasi 529 wa Rais Mohammed morsi


image

Watuhumiwa walihukumiwa kwa
makosa kadhaa ikiwemo mauaji ya
polisi
Mahakama nchini Misri
imewahukumu kifo watu 529 ambao
wanasemekana kuwa wafuasi wa
Rais aliyeng’olewa mamlakani
Mohammed Morsi.
Watu hao walikabiliwa ma mashitaka
mbali mbali yakiwemo mauaji ya
polisi pamoja uvamizi dhidi ya polisi.
Wafuasi hao wa chama kilichopigwa
marufuku, cha Muslim Brotherhood,
ni sehemu ya kundi lengine kubwa la
watu zaidi ya 1,200 wanaoaminika
kuwa wafuasi wa Morsi.
Maafisa wa utawala nchini Misri
wamekuwa wakiendesha msako
mkubwa dhidi ya wafuasi wa
vuguvugu hilo, tangu Morsi
kuondolewa mamlakani mwezi Julai
mwaka jana.
Maelfu wamekamatwa huku mamia
wakiuawa.
Mahakama hiyo ilitoa hukumu baada
ya vikao viwili pekee ambapo
mawakili wa watuhumiwa
walilalamika kuwa hawakupewa
muda wa kuwasilisha kesi yao
vyema.
Mauaji wanayodaiwa kufanywa na
watuhumiwa yalitokea Kusini mwa
Misri, mwezi Agosti, baada ya vikosi
vya usalama kuvunja kambi mbili za
wafuasi wa Morsi waliokuwa
wanataka arejeshwe mamlakani

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements