KESI YA OSCAR KUPIGWA KALENDA


image

Kesi ya mauaji ya mwanariadha
mlemavu wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius imeongezwa muda na sasa
itasikilizwa hadi May 16 kwenye
mahakama kuu ya Pretoria.
Pistorius alimpiga risasi na kumuua
mpenzi wake Reeva Steenkamp
kwenye Valentine’s Day mwaka jana.
Pistorius anajitetea kuwa alidhani
Reeva alikuwa kibaka aliyeingia
ndani mwake japo serikali inadai
hayo yalikuwa mauaji ya kudhamiria
ambayo ameyakana.
Kesi hiyo itakuwa na tarehe 7 na 11
April na itaendelea tena April 14 hadi
May 16. Hivi karibuni Pistorius
alipanga kuliuza jumba lake kifahari
la Pretoria ili kulipa gharama za
mawakili.
Kesi hiyo inaendelea Jumatatu hii.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements