NDEGE NYINGINE YA SHIRIKA LA NDEGE ZA MALAYSIA AIRLINE YATUA HONGKONG KWA DHARURA


image

Wakati bado juhudi zinaendelea bila
mafanikio za kuitafuta ndege ya
Malaysia Airlines aina ya Boeing
777-200 iliyopotea March 8 mwaka
huu ikiwa na abiria 239, ndege
nyingine ya shirika hilo imelazimika
kutua Hong Kong, china kwa dharula
baada ya hitilafu za umeme
kujitokeza ikiwa safarini.
Maafisa wa shirika hilo wameiambia
CNN mapema leo kuwa ndege hiyo
aina ya Airbus A330-300 iliyokuwa
ikitokea Kuala Lumpur kuelekea
Incheon, Korea Kusini ililazimika
kubadili njia na kwenda kutua kwa
dharula Hong Kong baada ya
wafanyakazi wa ndege hiyo
kugundua hitilafu katika genereta
inayozalisha umeme wa kawaida wa
ndege hiyo.
Kuala Lumpur ndio uwanja wa ndege
ilipotokea ndege ya shirika hilo
iliyopotea ambayo hadi sasa bado
haijaonekanekana.
Hata hivyo maafisa hao wameongeza
kuwa pamoja na hitilafu iliyojitokeza
lakini umeme uliendelea kuzalishwa
kupitia power unit ndogo ya ndege
hiyo.
SOURCE: MAIL ONLINE

Posted from WordPress for Android,by hailedavy