QCHILA ASEMA KUWA “SIFANYI MOVIE KUUZA SURA ”


Q Chillah amewataka watu na wadau
mbalimbali kutambua kuwa kufanya
kwake filamu sio kwa lengo la kuuza
sura au kukimbia majukumu yake ya
muziki.

image

Kutoka kushoto,Profesa Jay,Adam
Kuambiana,JB na Q Chillah wakiwa
maeneo ya Coco Beach hivi karibuni
Chillah amesema kuna watu
wanaodhani uamuzi wake wa
kufanya filamu umetokana na
kushindwa kufanya muziki.
“Hakuna kinachoshindikana katika
maisha,” ameiambia Bongo5. “Kama
kuna watu muhimu wananiambia
nifanye filamu nitaendelea kufanya.
JB na Adam Kuambiana Director
waliniambia kuna filamu ya kufanya
‘Hukumu Ya Ndoa Yangu’ na bado JB
aliambia niwe kwenye kampuni yake
Jerusalem ili tufanye mambo
makubwa zaidi ila nikamwambia
bado kwanza kwa sasa. Japokuwa
mimi si mtu wa filamu watu wengi
wanapenda nifanye filamu. Kwahiyo
nashangaa baadhi ya watu
wanadhani nimeenda kwenye filamu
kwaajili ya kuuza sura na kukimbia
majukumu yangu ya muziki. Jamani
mimi ni msanii Mkubwa sana na nina
uwezo mzuri wa kuimba na kufanya
vitu vizuri sana katika muziki.
Kwahiyo nitaendelea kufanya muziki
wangu mzuri na kama nitahitajika
kufanya filamu nitafanya.Lakini
maisha yangu nyuma ya pazia
naweza sana kufanya filamu vizuri
sana,na pia si biashara.”

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements