93•7 FM DARESSALAAM.ITAKUA NI ZAIDI YA BURUDANI


Baada ya kuwapa story kuhusu
ukweli juu ya requency za 93.7 FM
DSM ambazo zimeonekana kama
ujio mpya wa redio jijini Dar es
Salaam leo tunachimba zaidi juu ya
redio hiyo ambayo bado jina lake
halijajulikana. Katika fuatilia fuatilia
yetu tumefanikiwa kupata fununu
kuwa bado jina la kituo hicho
linafanyiwa kazi kwa kuwataka watu
wapendekeze jina wanaloona litafaa.

image

Zaidi ya hapo tumepata data ambazo
zinaonyesha mwanga katika mfumo
wa utangazaji wa kituo hicho kipya
kinachotegemewa kutingisha jiji pale
kitakapoanza kurusha matangazo.
Moja ya data hizo ni pamoja na
watangazaji wake ambapo wambea
wametudokeza tayari watangazaji
kibao pamoja na madj kutoka pande
tofauti za nchi ya Tanzania
wanasaka contact pamoja na kujua
mahali ofisi za kituo hicho zilipo ili
kuwasilisha maombi yao.
“Kitu cha kushangaza ni kwamba
katika listi hiyo inasemekaa majina
makubwa kibao katika tasnia
mbalimbali ikiwemo muziki, filamu
na michezo ni baadhi ya wanaotafuta
namba za simu na anuani za
wahusika kwaajili ya kupatanafasi,”
kilisema chanzo kimoja.
Jambo jingine ni kuhusu vipindi
ambapo inasemekana kituo hicho sio
tu kitakuwa kikijihusisha zaidi na
burudani, la hasha, bali kutakuwa na
segment nyinginezo nyingi ambazo
zipo nje ya ukanda wa burudani ila
watakuja na mfumo wa burudani
ambao haujatumiwa ama hautumiki
na vituo vingine vya redio hapa
Tanzania. Mambo ya siasa, afya,
michezo na vitu vingi vitakuwa pia
sehemu ya vipindi katika kituo hicho.
Kwa sasa wananchi kutuma playlist
zao ili waweze kuwa sehemu ya
mfumo huo mpya. Tutaendelea
kufuatilia kaa tayari kupata habari
zaidi kuhusiana na kituo hicho na
fuatilia twitter yao ya @New937.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements