HII NDIO KAULI YA MADEE BAADA YA TAMKO LA KTMA2014 KUHUSU KUINDOA NYIMBO YAKE KATIKA KINYAN’GANYIRO


image

Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA
limeziondoa nyimbo tatu kwenye
mchakato wa tuzo za muziki
Tanzania, KTMA kwa madai kuwa
zinakiuka maadili ya Kitanzania

image

Nyimbo hizo ni pamoja na
‘Nimevurugwa’ wa Snura, ‘Uzuri
wako’ wa Jux na ‘Tema Mate’ wa
Madee.
Akizungumza na Bongo5 leo baada
ya kupata taarifa ya kuondolewa
wimbo wake kwenye tuzo hizo,
Madee amesema hajapendezwa na
hatua hiyo.
“Sichukui hatua yoyote ila
nawashangaa tu hao viongozi ambao
wanahusika na mchakato mzima.
Sisi tunaandika nyimbo ambazo
vijana wetu wanazipenda,kwahiyo
kama wameamua hivyo basi wawe
wanatuandikia wao
nyimbo,kwasasabu sisi
tunawaandikia vijana wenzetu, sasa
unakuta hao wanaoendesha
mchakato ni wazee hawawezi
kuchanganua maneno yetu,ifike time
sasa wawe wanatuandikia mashairi,”
amesema Madee.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements