LatestNews: Idadi ya Vifo katika shambulizi la Bomu huko Mombasa yaongezeka.


image

Idadi ya waliofariki kufuatia
shambulio la Likoni imeongezeka na
kufikia 6 huku 9 waliokua wakipokea
matibabu wameruhusiwa kurudi
nyumbani na 6 hao walifariki
kufuatia majeraha ya risasi,Polisi
nchini Kenya imesema bado
hawajafutilia mbali uwezekano wa
kuwa lilikua shambulio la kigaidi.
Mwandishi wa habari kutoka Dw
nchini Kenya anaelezea kwa sasa
kinachoendelea Mombasa>>’Hali
ilivyo mjini Mombasa ni hali ya
kutatanisha kukosekana kwa
usalama kwa sababu kama
unavyojua tukio hili limezua hofu
sana hasa kwa wakazi wa mji huu
wa Mombasa’
‘Nakumbuka tukio la watu 5
waliuwawa kwenye kanisa moja
hapa Likonyi ni kitendo kilichotokea
siku 2 baada ya Waziri wa usalama
kutoa taarifa kwa wakazi wa hapa
kuwa usalama utadumishwa’
‘Hali ni tete hapa Mjini Mombasa
baada ya tukio hilo ambalo watu hao
waliuwawa msako wa polisi
uliendelea kuimarishwa kuanzia saa
8 na msako huo uliendelea usiku
kucha na taarifa tulizopokea kwa
sasa ni kwamba watu 59 wametiwa
nguvuni’
‘Wasiwasi upo kwa sababu hiki ni
kitendo kilichotengenezwa ndani ya
kanisa na unajua si mara ya kwanza
kitendo hiko kutokea hapa Mombasa
nakumbuka fujo zilizozuka baada ya
kitendo cha ugaidi kutokea hapa
Mombasa kuliokua na taharuki
miongoni mwa wakazi wake hasa
baina ya wakristo na waislam’
‘Hiki ni kitendo ambacho watu
wanahofia kimetekelezwa kuzua hofu
hasa miongoni mwa waumini wa dini
hizo mbili lakini viongozi wa kidini
wamekuja pamoja na kusema
kwamba hiki ni kitendo kilichofanywa
na magaidi tu ili kuzua mtafaruku
miongoni mwa waumini baina ya
wakristo na waislam hilo ni tukio
linaloendelea kuchunguzwa’
‘Hadi kufikia sasa hakujawa na
taarifa za kuthibitisha kitendo hiki
kilitekelezwa kwa malengo gani na
wakina nani hasa,hali ya wasiwasi
mjini Mombasa bado ipo na kama
unakumbuka kuwa tukio hili
limetokea siku chache baada ya watu
wawili kukamatwa wakiwa na
mabomu Mabomu ambayo
yaliharibiwa hivi juzi tu kwa hivyo ni
tukio linalozidi kutia hofu kwa wakazi
wa Mombasa’.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements