SERIKALI TATU YAZUA MAZITO ZANZIBAR!


Serikali 3 yaibua mazito Zanzibar

image

WANACHAMA wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Zanzibar,
wametakiwa kuacha tabia ya
kuwataja watu wenye asili ya
Pemba pekee kuwa ndio wenye
msimamo wa kudai Serikali tatu,
bali mfumo huo umependekezwa
na watu wenye asili tofauti.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
wa Chipukizi wa CCM, Bw. Muhija
Ali Kombo, katika kongamano la
wana CCM lililofanyika mwishoni
mwa wiki iliyopita, Mtoni Wilaya
ya Magharibi Unguja.
Alisema imekuwa kawaida kwa
baadhi ya wanachama wa chama
hicho kuwaandama watu
wenye asili ya Pemba na kudai
wao ndio wanaotaka Serikali tatu
ambapo baadhi ya watu kutoka
Chaani, Makunduchi na Kitope
wanashabikia mfumo huo.
“Mimi mwenyewe ni Mpemba
lakini sishabikii mfumo wa
Serikali mbili sasa unaposimama
na kumtaja Mpemba kuwa ndo
anayeshabikia
Serikali tatu unafanya kosa,”
alisema.
Katika kongamano hilo, Bw.
Muhija aliwataja baadhi ya
viongozi ambao wana asili ya
Unguja
lakini wapo CCM pia ni waumini
wakubwa wa Serikali mbili.
Aliwataja viongozi hao kuwa ni
Mwakilishi wa Jimbo la
Kwamtipura, Bw. Hamza Hassan
Juma, Jimbo la Kitope Bw.
Mbarouk Makame Mshimba na
Jaku Hashim Ayuob ambaye ni
mwakilishi wa
Jimbo la Muyuni.
“Nimelazimika kuwataja kwa
majina kwa sababu ya uchungu
nilionao, kila mmoja wetu
anaposimama anatajwa Mpemba
lakini mimi, Mwnyekiti wa CCM
Mkoa wa Magharibi Bw. Yussuf
Mohammed na Bw. Baraka
Shamte ni wapemba lakini mbona
hatushabikii mfumo wa Serikali
tatu,” alisema.
Katika kongamano hilo,
wanachama hao walitoa azimio la
kuwataka wabunge na
wawakilishi
wa CCM kusimama imara na
kutetea mfumo wa Serikali mbili
vinginevyo watakaporudi
watafute
majimbo mengine ya kugombea
2015.
Kongamano hilo liliandaliwa na
CCM likiwa na lengo la kutoa
maazimio yao juu ya muundo wa
Muungano likitarajiwa kuendelea
katika Mkoa wa Kaskazini Machi
29 mwaka huu.
chanzo;Majira

Posted from WordPress for Android,by hailedavy