TANGAZO LA SERIKALI: YAHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO KATIBA!


image

Mhe. Rais aliunda Tume ya
Mabadiliko ya Katika kwa mujibu
wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya
83 kwa Tangazo la Serikali
Na.110 la Mwaka 2012.
Tume ilikusanya maoni na
kuandaa Rasimu ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambayo imewasilishwa
kwenye Bunge Maalum.
Kwa mujibu wa kifungu cha 31
cha Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa
mamlaka ya
kuvunja Tume ya Mabadiliko ya
Katiba baada ya Rasimu ya Katiba
kuwasilishwa Bungeni.
Mnamo tarehe 18 Machi, 2014
Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji
Joseph Sinde Warioba aliwasilisha
Rasimu ya Katiba kwenye Bunge
Maalum.Kutokana na hatua hiyo,
na kwa mujibu wa kifungu cha 31
cha Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Rais wa Jamhuri ya
Muungano alivunja rasmi Tume
ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19
Machi,2014 kwa Tangazo la
Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi,
2014.
Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli
zote za Tume ya Mabadiliko ya
Katiba zimemalizika rasmi tarehe
19 Machi, 2014.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam.
25 Machi,2014
TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU
KUVUNJWA KWA TUME YA
MABADILIKO YA KATIBA

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements