GAZETI LA UBELIGIJI LAOMBA LADHI KWA KUMDHIHAKI RAIS OBAMA NA MKEWE


image

Gazeti la De Morgen nchini Ubelgiji
limeomba radhi kwa kitendo chake
cha kuchapisha picha na maneno
yaliyohashiria vitendo vya ubaguzi
wa rangi kwa Rais wa Marekani,
barack Obama na mkewe Michelle.
Picha hiyo inamuonyesha Rais
Obama na mkewe wakiwa kwenye
maumbo ya nyani huku picha
nyingine ikiwa na ujumbe
uliosomeka, ”FIRST BLACK
PRESIDENT OF THE USA, STARTS
SELLING WEEDS”.
Kwa mujibu wa mtandao wa Al
Jazeera ulidai kwamba, sehemu ya
picha hiyo waliongezea utani
uliosema, Rais wa Urusi Vladimir
Putin amekubaliana na picha hiyo
ingawa hapo baadae walijishtukia na
kuwahi kuomba msamaha ikiwa ni
siku moja kabla ya rais Obama kutua
nchini humo kwenye moja ya ziara
zake barani ulaya.
Je, De Morgan ni wabaguzi?ambapo
walikiri utani haukuwa mzuri na
walielezea kwamba tulifanya makosa
kudhania ubaguzi wa rangi
haukubaliki na kwa njia hii ilikuwa ni
moja ya mzaha”. waliandika gazeti
hilo katika moja ya hatua
walizochukua za kuomba radhi kwa
kitendo walichofanya.
Hata hivyo haikuchukua muda mrefu
kwa wafuasi wa mtandao wa Twitter
kuanza kulishambulia gazeti hilo
huku watu wengi wakihoji ni nani
aliyepewa kibali cha kuchapisha
gazeti hilo na pande nyingine
kuibuka na kudai kuwa ilikuwa ni
mzaha.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements