VITAMBUE VYUO VILIVYO FUTWA NA WIZARA YA ELIMU


image

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi imekunjua
makucha yake kwa kutangaza
kuvifuta vyuo 10 ambavyo
havikusajiliwa na Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) .
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Philip
Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es
Salaama mbele ya Kamati ya Bunge
ya Huduma za Jamii na kuongeza
kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni
kutokana na kutokufuata utaratibu
wa kusajiliwa.
Alivitaja vyuo hivyo ni Media and
Research Center, Vision Hotel and
Tourism College, East Africa College
of Hospitality and Tourism, The
Africa Institute of Business
Management na Aspiration Training
Center, vyote vya Dar es Salaam.
Vingine ni Dar es Salaam School of
Hair Design, Media and Values
Training Institute na Information
Technology Training Center vya Dar
es Salaam. Pia alikitaja Chuo cha
Morogoro School of Medical Sciences
cha Morogoro.
Katika hatua nyingine, Mulugo alikiri
kuwa kuna upungufu katika kutoa
mikopo kwa wanafunzi wa vyuo
vikuu kupitia bodi ya mikopo.
Alisema kuna changamoto nyingi
zinazoikabili bodi hiyo zikiwamo
urejeshwaji wa mikopo kwa
wanafunzi waliomaliza chuo, mfumo
wa utoaji wa mikopo, ufinyu wa
bajeti na makosa yanayotokana na
wanafunzi kukosea kujaza fomu za
mikopo

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements