ALICHOSEMA ALI KIBA KUHUSU WIMBO WA “ROSA ”


image

Siku kadhaa baada ya kusambaa
wimbo ulioaminika kuwa ni wa Ali
Kiba ukiwa na jina la Rosa, mwimbaji
huyo ameukana wimbo huo na kudai
hafahamu lolote kuhusu wimbo huo
na hata hajawahi kuusikia.
“Nyimbo zipo lakini sija release
nyimbo, sijatoa nyimbo so far na sijui
nani ameimba na sijawahi hata
kuusikia.” Amesema Ali Kiba.
Mwimbaji huyo ameongeza kuwa
watu wameona yuko kimya na
wameamua kutoa wimbo kwa jina
lake kitu ambacho hakina mantiki na
kwamba anadhani watu hao
wamefanya makusudi au wametumia
sayansi ya sauti ku-fake sauti yake.
Amesema hajui lengo la mtu
aliyefanya, “I think ni trick moja
ambayo imefanywa sielewi na nani
lakini I don’t know if in a good way or
bad way”.
Ameiweka positively pia kuwa
huenda aliyeiimba ni mtu
anaemkubali yeye kama role model
wake.
Credit: Renatus Kiluvya

Posted from WordPress for Android,by hailedavy