KUHUSU NCHINI UTURUKI (TURKEY ) KUFUNGIA YOUTUBE


image

Uturuki imeufungia mtandao wa
Youtube, siku chache baada ya
kuifungia pia Twitter baada ya
mitandao hiyo kutumika kusambaza
sauti iliyorekodiwa na inayouweka
usalama wa nchi hiyo pabaya.
Hatua hiyo ilikuja saa chache baada
ya kusambaa kwa sauti kwenye
mtandao wa Youtube, zilizokuwa za
mkutano wa usalama wa viongozi
wakubwa wa serikali kuhusu hatua
za kijeshi ndani Syria.
Waziri Mkuu, Tayyip Erdogan jana
aliwashutumu wapinzani kwa kuvuja
kwa sauti hiyo.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements