SHAMBULIO LA KIGAIDI LAUA SITA(6) KENYA


image

Watu sita wameuawa na wengine
wengi kujeruhiwa katika shambulizi
la kigaidi katika eneo la California
mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi.
Polisi wamesema kuwa milipuko
miwili ilitokea wakati magaidi
waliporusha mabomu katika
mkahawa mdogo ulio karibu na kituo
cha mabasi mtaani humo.
Walioshuhudia shambulizi walisema
kuwa walisikia mlipuko wa tatu
katika eneo hilo ingawa polisi
hawajathibitisha hilo.
Miongoni mwa waliojeruhiwa
walikuwa wanawake ambao walipata
majeraha mabaya na kukimbizwa
hospitalini kwa matibabu.
Kwa mujibu wa polisi wale
waliouawa walikuwa wamekwama
ndani ya mkahawa huo baada ya
mlango kufungwa na washambulizi
waliorusha mabomu hayo ndani ya
mkahawa wenyewe.
Waathiriwa walikuwa wameenda
kununua chakula cha jioni.
Inaarifiwa washambuliaji walitumia
maguruneti au mabomu ya
kutengezwa nyumbani kufanya
mashambulizi hayo.

Posted from WordPress for Android,by hailedavy