W. H. O KUDHIBITI EBOLA NCHINI GUINEA


image

Watu 122 wamembukizwa homa hiyo
kali kufika sasa Afrika Magharibi
Shirika la afya duniani limesema
linachukulia kwa uzito sana mlipuko
wa sasa wa homa ya Ebola
Magharibi mwa Afrika.
Kufikia sasa shirika la WHO
limethibitisha visa 122 vya homa ya
Ebola huko Guinea na vingine saba
katika nchi jirani ya Liberia.
Hadi sasa watu 80 wamefariki
kufuatia maambukizi hayo wengi
kutoka Guinea na wanne wakiwa raia
wa Liberia.
Huku juhudi zikiendelea kudhibiti
homa hii angamizi inayowaua
asilimia 95 ya wanaoambukizwa,
WHO imeanza kuwachunguza mamia
ya raia nchini Guinea.
Shirika hilo limeanza kutuma nguo za
kukinga maambukizi pamoja na
maafisa wa afya.
Hii ndio mara ya kwanza eneo hilo
kushuhudia mulipuko wa homa ya
Ebola.
Mara ya kwanza Homa hiyo kuzuka
Afrika ilikua mwaka 1976 katika
mataifa ya Sudan na iliyokua Zaire
kwa sasa Jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Congo.
Huambukizwa kupitia damu na maji
ya mwili pia inaweza kuambukizwa
kati ya binadamu na wanyama.
Siyo rahisi kutambua Ebola na
maafisa wa afya wanaowahudumia
wagonjwa wanakumbwa na hatari ya
kuambukizwa.Rais wa Guinea
amewataka raia kutokua na hofu
akisema hatua zote zimechukuliwa
kukabiliana na maradhi haya.

image

Posted from WordPress for Android,by hailedavy

Advertisements